Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa
Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin Walsh.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. Aidhaa, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, kiuchumi na kisiasa baina ya Tanzania na Marekani. Viongozi hao wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha mahusiano yaliyopo katika nyanja mbalimbali kwa faida ya Nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na
Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin Walsh. Pamoja nao ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi akifuatilia mazungumzo hayo.
Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi
Modest Mero (katikati) akifuatilia mazungumza ya Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) akiwa katika
mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin Walsh.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
Kabudi (Mb) akiagana na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi
Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin Walsh baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.