PanAfrican Energy Tanzania (PAET), kampuni inayoongoza katika uzalishaji na usambazaji wa gesi nchini, ilipata changamoto ya kukatika kwa usambazaji wa gesi asilia (CNG) katika kituo chao cha Ubungo jijini Dar es Salaam, kutokana na hitilafu katika mtambo wa mfumo wa kubana gesi.
Huduma ya gesi ya CNG hutolewa kwa wateja kadhaa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na madereva wengi ambao wamebadili magari yao ili kutumia mfumo wa gesi.
Hadi kufikia jana jioni ya tarehe 28 September, PAET ilifanikiwa kurekebisha hitilafu hiyo na inayo furaha kutangaza kuwa sasa huduma zimerudi kama kawaida katika kituo hicho.