Waziri wa maliasili na utalii ,Balozi Dk Pindi Chana akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo jijini Arusha Leo.
Waziri wa maliasili na utalii Balozi Dk Pindi Chana akimkabithi vitendea kazi Mkuu wa majeshi mstaafu Jeneral Venance Mabeyo ambaye ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, baada ya kuzinduliwa kwa bodi hiyo leo jijini Arusha.
**************************
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Waziri wa maliasili na utalii Balozi Dk Pindi Chana amezindua rasmi bodi ya wakurugenzi mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro huku akiwataka kusimamia kikamilifu mamlaka hiyo sambamba na kuongeza maeneo mapya ya uwekezajiili kuongeza pato la Taifa.
Chana ameyasema hayo leo wakati akizundua bodi hiyo jijini Arusha huku akiitaka bodi hiyo kusimamia ipasavyo shughuli za mamlaka hiyo sambamba na kuweka mikakati mipya itakayosaidia mamlaka hiyo kuendelea kukua zaidi.
Amesema kuwa ,mkakati wa serikali ni kuongeza watalii hadi kufikia takribani watalii milioni 5 kwa mwaka 2025,hivyo waweke mikakati zaidi kuhakikisha wanafikia malengo hayo,huku akiwataka
kuimarisha utalii nyanda za juu kusini ili wananchi waweze kunufaika zaidi na fursa mbalimbali .
Dk Chana amesema kuwa, mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro hivi sasa inachangia mapato makubwa kwa takribani asilimia 17 ,hivyo ameitaka bodi hiyo kuweka mikakati zaidi na kuweza kuvuka malengo hayo .
” tuchukulie mfano kwa mwaka 2019/2020 kabla ya mlipuko wa Uviko 19 eneo la mamlaka lilitembelewa na zaidi ya wageni laki 7 na kupata mapato ya shs 123 bilioni, hivyo kutokana na changamoto ya uviko19 idadi ya wageni ilishuka hadi kufikia wageni laki moja tisini na moja na kupata mapato ya shs 31.4 bilioni kwa kipindi cha mwaka 2020 /2021″amesema Dk Chana.
Ameongeza kuwa,baada ya serikali kutangaza vivutio kupitia filamu ya Royal Tour iliyotangazwa na Mhe Rais Samia Suluhu imeweza kuongeza idadi na kufikia zaidi ya wageni laki nne ishirini na tano na fedha kuweza kuongeza hadi kufikia bilioni 91.1 kwa mwaka 2021 hadi 2022.
Naye Mwenyekiti wa bodi hiyo Mkuu wa majeshi mstaafu Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa,watahakikisha wanafanya kazi kwa uaminifu na kuhakikisha mamlaka hiyo inakuwa bora kimataifa.
Amesema kuwa, watahakikisha wanahamasisha watalii wa ndani kuweza kutembelea mamlaka hiyo huku wakiahidi kufikia malengo yaliyowekwa ya kufikia idadi ya milioni 5 .
“Tutahakikisha tunabuni mazao mapya ya utalii na tunaahidi kusimamia kwa ufanisi zoezi la wananachi kuhamia kijiji cha Msomera na tutafanya zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa ili azma ya wizara iliyopangwa itimie”amesema Jenerali Mabeyo.
Kwa upande wake,Msajili wa hazina Benedicto Mgonya amesema kuwa,bodi ya wakurugenzi ndo chombo kinachoongoza hivyo amewataka kuwa na mfumo madhubuti katika kuhakikisha mamlaka hiyo inazidi kuimarika.
Aidha amewataka kusimamia mamlaka hiyo kwa kuzingatia sheria na miongozo inayotolewa na kutoa taarifa za utendaji wake na kwa kufanya hivyo itaongeza ufanisi katika utendaji kazi na kufikia malengo mbalimbali yaliyowekwa.