Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa ndani ya kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited kinachojishughulisha na uzalishaji wa nyaya na kebo za umeme mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo Septemba 27,2022 Kigambo Jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile akiwa pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiangalia baadhi ya nyaya za umeme ambazo zimezalishwa na kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited wakati walipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho leo Septemba 27,2022 Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile akiwa pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiangalia baadhi ya nyaya za umeme ambazo zimezalishwa na kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited wakati walipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho leo Septemba 27,2022 Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile (katikati) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangasa (wa kwanza kushoto) pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza walipotembelea Kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited kukagua ni namna gani wanahifadhi mazingira. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile (wa pili kushoto) akiongozana na kamati hiyo wakiwa kwenye kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited kukagua ni namna gani wanahifadhi mazingira.Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza akimuuliza jambo Mhandisi Viwango wa Kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited Mhandisi Delain Mwakalasi mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira kutembelea kiwanda hicho leo Septemba 27,2022 Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira imekipongeza kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited kinachojishughulisha na uzalishaji wa nyaya na kebo za umeme kwa kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu za utunzaji wa mazingira.
Pongezi hizo zimetolewa leo Septemba 27,2022 na Mwenyekiti wa Kamati Mhe.David Kihenzile katika ziara ya kamati hiyo kwenye kiwanda hicho kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ziara hiyo Mhe.Kihenzile amesema wameridhishwa na kiwanda hicho kwani hakitoi gesi chafu, maji taka au taka ngumu ambazo zinaweza kuwa kero na kuathiri wananchi ambao wanaishi karibu na kiwanda hichio.
“Tumeridhishwa na mpango wa uhifadhi wa mazingira kwenye kiwanda hiki na tunawasihi viongozi na wafanyakazi wa kiwanda kuendelea kufanya vizuri katika utunzaji wa mazingira kwenye eneo hili la kiwanda”. Amesema Mhe.Kihenzile.
Aidha ametoa wito kwa viwanda vingine viendelee kufanya vizuri katika suala la uhifadhi wa mazingira ili kuepukana na mlipuko wa magonjwa hatarishi yatokanayo na uchafuzi wa mazingira kwenye viwanda vyetu.
Pamoja na hayo Mhe.Kihenzile ameipongeza NEMC kwa kuhakikisha viwanda vinavyozalisha bidhaa nchini vinafuata Sheria,taratibu na kanuni za uhifadhi wa mazingira.
Nae Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza amesema hawajapata taarifa ya malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu kero za kiwanda hicho hivyo amewapongeza kwa kuzingatia uhifaddhi na utunzaji wa mazingira kwenye eneo hilo.
Hata hivyo ametoa maelekezo kwa uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanatoa msaada kwa wannachi ambao wanaishi karibu na kiwanda hicho kwa kujenga miradi mingine mikubwa ikiwemo miradi ya maji, elimu, afya na miradi mingine mingi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa sheria ya Mazingira (NEMC, Mhandisi Redemka Samweli amesema watahakikisha wanasimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu kuboresha utunzaji wa mazingira kwenye kiwanda cha Elsewed Electric East Africa Limited.