Mtendaji Mkuu wa Tarura, Victor Seif,akizungumza na waandishi wa habari katika banda la taasisi hiyo wakati wa siku ya maadhimisho ya wahandisi nchini.
………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), imeanza mkakati wa kutengeneza barabara na madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe ambayo inaokoa gharama kwa asilimia 50..
Hayo yamesemwa leo Septemba 22,2022 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Tarura, Victor Seif wakati wa siku ya maadhimisho ya wahandisi nchini.
Mhandisi Seff amesema teknolojia hiyo itapunguza gharama kwasababu hutumia marighafi ambazo zinapatikana katika maeneo husika
“Gharama ni zaidi ya 50 zinapungua, ukitumia zege na nondo utakuta ni gharama zaidi ya mara mbili kama utakijenga kwa kutumia zege na nondo. Teknolojia hii wanatumia saruji, mchanga na mawe,”amesema Mhandisi Seff
Amesema wameshajenga mawe katika madaraja zaidi ya 72 mkoani Kigoma kwa Sh1.4 na kwamba ujenzi huo unaendelea kwenye mikoa Mwanza, Iringa na Singida.
Amefafanua kuwa mkakati huo utaangalia tunaangalia maeneo yote yenye mawe ambayo yatahusika katika ujenzi ambapo kwa kushirikiana na wafadhiri kutoka ubeligiji tunaanza kufundisha mafundi katika kujenga madaraja na sasa wapo kigoma wanafanyiwa mafunzo na wakirudi katika maeneo yao nao wetafundisha wengine.
Naye Mhandisi wa TARURA Makao Makuu Mhandisi Pharles Ngeleja amesema mipango iliyopo ni kuhakikisha wanawezesha mafunzo kwa wahandis ili waweze kufahamu kwasababu wao ndio wasimamizi wa miradi..
Amesema kuwa kuanzia ifikapo Februari mwakani kutakuwa na mafunzo ambayo yatafanywa na watu kutoka ubeligiji.
“Kuanzia Februari mwaka huu, tutakuwa na mafunzo yatakayofanyiwa na wenzetu wabeligiji, tutaanzia mikoa kadhaa na baadaye tutasambaa nchini,”amesema.