*****************************************
Shirika la Best-Dialogue ambalo limekuwa likifanya kazi na taasisi mbalimbali hapa nchini ambapo moja ya taasisi ambayo imekuwa ikifanya nalo kazi kwa karibu ni taasisi ya TCCIA ambako mpaka sasa mkataba umekwisha baada ya kufanya kazi kwa miaka 15.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam katika sherehe za kumaliza mkataba huo, Afisa Mtendaji wa taasisi ya TCCIA mkoa wa Katavi, Bw.Laban Ndimubenya amesema kuwa Best-Dialogue wamekuwa msaada mkubwa katika nchi kwasababu wamekuwa karibu sana na wao na kufanya kazi pamoja kwa ushirikiano mzuri.
“Sera nyingi zimefanyiwa mapitio, marejeo, mabadiliko kutegemeana na jinsi inavyoonekana inafaa baada ya majadiliano katika kuboresha mazingira ya kibiashara”. Amesema Bw. Ndimubenya.
Kwa upande wake Afisa habari na Mawasiliano wa baraza la kilimo na Mifugo Tanzania (ACT), Bi.Milly Sanga amesema wao wamenufaika na Best-Dialogue mara nyingi wamefanya majadiliano na serikali lakini majadiliano hayo hayaendi katika hali ya kawaida lazima wafanye utafiti ambao wanakuja na matokeo ya utafiti na wanayawasiliasha kwa serikali.
“Tumefanya utafiti katika masuala ya pamba, masuala ya ufugaji, masuala ya pembejeo feki pamoja na ushuru wa mazao. Utafiti wote huo umekuwa ukifadhiliwa na Best-Dialogue ambao mradi unaenda kuisha lakini kitu ambacho tumenufaika nacho ni pamoja na kutujengea uwezo na fursa ya kukaa na serikali kujadiliana nao kwa kutumia mbinu ambazo tulikuwa tunafundishwa”. Amesema Bi. Milly.