Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Bakwata Taifa, Sheikh Ally Hamisi Ngorike akizungumza.
Mlau akizungumza wakati akiwatambulisha wageni mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
Dotto Mwaibale na Philemon Mazala, Singida
MUFTI wa Tanzania Sheikh Dk. Abubakar Zubeir Ally Mbwana ameongoza maelfu
ya waislam mkoani Singida katika hafla ya kuzindua Mfuko wa Maendeleo wa Mufti
ambao ni muhimu kwa maendeleo ya waislam nchini.
Akizindua mfuko huo leo Septemba 19, 2022 katika hafla iliyofanyika Stendi
ya Mabasi ya Zamani mjini hapa Mufti Zubeir aliwataka waislam kote nchini
kujenga tabia ya kujitolea na kutoa kwa kile walichonacho kwa ajili ya
kuendeleza dini ya kiislam.
Alisema Mtume Muhammad (SAW ) alipokuwa akiutangaza uislam na kuukumbatia
kila aliyekuwa nacho alitoa halikadharika na waliokwenda hija walifanya hivyo
mpaka uislam ukafika ulipofikia.
“Watu walitoa mali zao mbalimbali kwa ajili ya kuipigania dini ya kiislam hivyo na sisi tusiwe nyuma
kufanya hivyo” alisema Mufti Zubeir.
Alisema jambo hilo la kuchangia mfuko huo si la ujanja ujanja bali lina mpango
kamili hivyo watumie fursa hiyo kwa ajili ya kutoa kwa maendeleo ya waislam na
dhawabu zao watazikuta mbele ya Mwenyezi Mungu.
Mufti Zubeir aliwahimiza waislam kufanya hivyo kwani Mungu ataona, waislam
wataona na Mtume Mohamad ( SAW)ataona na akaeleza kuwa waislam hawatakiwi kuwa na
tabia ya kuombaomba na kuwa ni heri ya kuwa na mkono wa kutoa kuliko wa
kupokea kwani waislam wa Tanzania ni matajiri ambao kilammoja hashindwi kutoa Sh.10,000
kwa mwezi kama alivyo jitolea mwanamke Hadija anaye simuliwa katika kitabu
kitakatifu cha quran.
Mufti Zubeir aliwataka waislam kuondoa dhana ya kuwa michango inayotolewa haiendi kufanya maendeleo badala yake wawe na imani akitolea mfano baadhi ya wenzao ambao
hakuwataja kuwa wamekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutokuwa na mtazamo huo.
“Wenzetu wakizungumza jambo wanakusanya pesa na wakiamua linakuwa, mimi nina ushahidi ipo siku nitawaambia lakini sisi tukizungumza jambo na Imam msikitini, baadhi ya viongozi kwenye kata, wilaya na mkoa wanalipinga” alisema Mufti.
Alisema kumekuwa na changamoto ya
watu waliostaafu au kuondolewa kazini
kwenda misikitini na kujifanya wanajua kila kitu “wataaalam’ huku
wakizungumza kiingereza na kuwavuruga waislam ambapo alieleza kuwa jambo hilo sio zuri.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mkuu wa Wilayaya Singida,
Mhandisi Paskas Mulagiri alisema Serikali imekuwa ikiamini kwa sehemu kubwa
sana kuwa amani na utulivu uliopo hapa nchini ni kwa sababu ya kazi kubwa
inayofanywa na viongozi wa dini kwa kuliombea taifa na maadili ya kidini ambayo
yanajenga amani na upendo.
Muragili alitumia nafasi hiyokuwashukuru viongoziwa dini kwa kushirikiana
na Serikali katika kuhamasisha waumini wao kwenye zoezi la kitaifaa la Sensa ya
Watu na Makazi ambalo lilipata mafanikio makubwa na Mkoa wa Singida ulipata zaidi ya asilimia 100.
Aidha Muragili alimpongeza Mufti wa Tanzania Sheikh.
Dk.Abubakar Zubeir kwa kuwa na maono ya kuanzisha Mfuko wa Maendeleo wa Mufti
(MDF) ambao ni mkombozi mkubwa kwa Serikali kwani unakwenda kutatua changamoto
mbalimbali za wananchi.
Katika uzinduzi wa mfuko huo viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam,
Serikali, wafanyabiashara, watumishi wa umma, watu binafsi, wananchi na wanasiasa walijitokeza kuchangia mfuko huo miongoni mwao akiwa ni Bi. Salha Amir mkazi wa Iramba ambaye ameitoa Hospitali yake yenye vyumba zaidi ya 25 na ardhi
yenye ekari 12.5 vyote vikiwa na thamani ya Sh.Bilioni 1 kwa ajili ya mradi wa
mfuko wa maendeleo wa Mufti.
Wengine waliochangia mfuko huo ni Mwenyekiti wa Bakwata Mkoa wa Singida,
Jumanne Nkii ambaye naye alitoa nyumba ya vyumba saba na eneo la ardhi na
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu ambaye ametoa ahadi ya
kutoa Sh.10 milioni akishirikiana na rafiki zake wadau wa maendeleo pamoja na
Ahmed Misanga ambaye ni Mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida
kutoka Kata ya Ihanja na Mjumbe wa Halmashauri Bakwata Mkoa wa Singida ambaye alitoa Sh.300,000.