NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amesema wanalitafuta gari aina ya IST ambalo linadaiwa kutumika na mtu mwenye asili ya kiarabu kumchukua mwanafunzi wa shule ya sekondari Tumbi ,kidato cha pili ambae walizunguka nae hadi Mlandizi na kwenda kumtelekeza Ubungo.
Alitoa rai hiyo ,wakati akizungumza na wanafunzi ,wazazi na walimu wa shule ya msingi Kibaha Indepent (KIPS).
Alisema nia na madhumuni ya watu hao haijajulikana bado kwani hawajamdhulu mtoto huyo.
Alieleza vyombo vya dola vipo kazini kilisaka gari hilo na mtu ama watu hao ili kuwachukulia hatua za kisheria.
Ndikilo aliwaonya watoto hususan wanafunzi kuacha tabia ya kuomba au kupewa rift ama kupakiwa katika magari wasiyoyajua ili kuepuka kutekwa au kupata madhara.
Pia aliwaomba wazazi na walezi kusaidiana kuwakanya watoto wao kuacha kupenda rift .
“Tunawapa salamu watu hao waliofanya tukio hilo ,kwamba wajue watakimbia ila tutawakamata kwani haijulikani dhamira yao kuchukua watoto wa watu kuwazungusha na kwenda kuwatelekeza mbali “alisema Ndikilo.