Mwenyekiti wa Sauti ya wapinga Rushwa Mkoa wa Dodoma,ambaye ndio mratibu wa mbio hizo,Haruna Kitenge,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya mashindano ya Sepesha Rushwa Marathon yanayotarajia kufanyika Disemba 11,2022 jijini Dodoma .
……………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
JUMLA ya washiriki 2000 wanatarajia kushiriki mashindano ya Sepesha Rushwa Marathon yanayotarajia kufanyika Desemba 11 mwaka huu Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Sauti ya wapinga Rushwa Mkoa wa Dodoma,ambaye ndio mratibu wa mbio hizo,Haruna Kitenge amesema washiriki hao ni wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo,watumishi wa serikali na taasisi mbalimbali pamoja na wakimbiaji mbalimbali.
Kitenge amesema mbio watakazokimbia ni Km 21,10,5 na 3 lengo la mashindano hayo ni kuwaelewesha vijana kuhusu madhara ya rushwa pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeleza kampeni ya Sepesha Rushwa katika Jiji la Arusha.
Pamoja na hayo Kitenge aziomba kampuni,taasisi binafsi na mashirika kujitokeza kudhamini mbio hizo.
Huku Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dodoma,Robert Mabonye akiwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kushiriki mbio hizo ambapo amesema hiyo