Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akiwapungia mikono wananchi jana wakati akiwasili Wilaya ya Ikungi mkoani Singida akitokea Dodoma ambako aliapishwa na kuhudhuria
vikao vya bunge kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Wanafunzi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mtaturu akipita juu ya kanga zilizo tandazwa na wakina mama.
Burudani zikiendelea
Burudani zikiendelea
Kikundi cha Sanaa cha Liti kikimuimbia Mbunge Mtaturu (kushoto aliyebeba kibuyu) wimbo maarumu wa kabila la Wanyaturu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ali Mwanga akizungumza kwa niaba ya madiwani wa halmashauri hiyo.
Mchungaji Jeremia Samwel Mpepho akiombea mkutano huo.
Maulid Ali Mohamed akiuombea dua mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza kwenye mkutano huo.
Watoto nao walikuwepo kwenye mkutano huo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Noverty Kibaji, akizungumza. |
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akizungumza
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akihutubia wananchi.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji , Juma Aweso akihutubia.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Juma Aweso (kushoto) akiwatambulisha baadhi ya maofisa wa wizara hiyo watakao piga kambi ya kutatua changamoto ya maji katika jimbo hilo. (Wa pili kushoto ni Mbunge Miraji Mtaturu
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa akimkabidhi kadi ya chama hicho, Venance Elias aliyekuwa ni Mwenyekiti wa Chadema Kijiji cha Ighuka ambaye amehamia CCM.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Likapakapa akimpatia kadi Peter Zacharia aliye hamia CCM akitokea Chadema. Zacharia alikuwa ni Katibu wa Vijana wa Chadema Kata ya Ihanja. Katika mkutano huo makada 11 kutoka CUF na Chadema walihamia CCM.
Na Dotto Mwaibale, Singida
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso amewaagiza maofisa watatu wa wizara hiyo kupiga kambi Jimbo la Singida Mashariki ili kuanza kukabiliana na changamoto ya maji baada ya Rais Dkt.John Magufuli kutoa sh.bilioni mbili.
Aweso alitoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kumpokea Mbunge wa jimbo hilo, Miraji Mtaturu wakati akitokea bungeni Dodoma ambako aliapishwa na kuhudhuria vikao vya bunge kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuongoza jimbo hilo lililokuwa likiwakilishwa na Mbunge Tundu Lissu (Chadema)
” Nina waagiza maofisa watatu wa wizara ya maji kubaki katika jimbo hili ili kuanza hatua za awali za kumaliza changamoto ya maji na sisi kama wizara tutahakikisha inakwisha” alisema Aweso.
Maofisa ambao watapiga kambi katika jimbo hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (SUWASA) Mkoa wa Singida, Mhandisi Patrick Nzamba, Mhandisi Genes Kimaro kutoka Wakala wa Usambazaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida ( RUWASA) na Mhandisi Hopeness Liundi kutoka Ruwasa Wilaya ya Ikungi.
Aweso alisema tayari Rais Dkt. John Magufuli amekwisha toa sh.bilioni mbili kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji hivyo kama wizara watahakikisha suala hilo linabaki kuwa ni historia.
Mbunge Miraji Mtaturu akihutubia katika mkutano huo alitaja vipaumbele vyake vitatu kuwa ni elimu, maji na afya pamoja na uchumi ambapo alisema kila mwaka atawasaidia kuwanunulia sare za shule wanafunzi 200, 100 wakiwa wa shule za sekondari na 100 wengine wakiwa ni wa shule za msingi.
Aliongeza kuwa kila mwaka atawalipia ada wanafunzi 10 watakaoingia kidato cha tano watano wakiwa wakike na watano wengine wakiwa wavulana pamoja na kutoa elimu ya kuutunza utamaduni wa kabila la Wanyaturu.
Akizungumzia maji alisema tayari Serikali ilikwisha wasaidia kuchimba visima 28 na imekwisha toa fedha hizo sh. bilioni mbili zilizotolewa na Rais, na katika suala la uchumi alisema ataanzisha mradi wa kukopesha ng’ombe wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumzia suala la usalama kuelekea uchaguzi wa viongozi wa serikali za mtaa alisema wananchi wasiwe na wasiwasi kwani wamejipanga vizuri na kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa shwari wakati wote.