Na Mwandishi Wetu, MWANZA
TIMU ya Kagera Sugar ya Bukoba imeipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Mbao FC jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua, Kagera Sugar walitangulia kwa bao la Ally Ramadhan dakika ya 20, lakini Hebert Lukindo akaisawazishia Mbao FC dakika ya 60.
Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Mecky Mexime imemaliza nafasi ya 19 kwa pointi zake 44 sawa na Stand United ilyomaliza nafasi ya 18 na Mwadui FC ya 17 kwa wastani wao nafuu wa mabao.
Kagera Sugar inaungana na African Lyon ya Dar es Salaam iliyoshika mkia kuipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu baada ya zaidi ya miaka 20 ya kushiriki mfululizo ligi hiyo.
Nazo Stand United ya Shinyanga, maarufu kama Chama la Wana’ na Mwadui FC ya Shinyanga zitamenyana na timu za Daraja la Kwanza, Pamba SC na geita Gold kuwania kubaki Ligi Kuu katika mechi za mchujo.
Stand United imechapwa mabao 2-0 na JKT Tanzania 2-0 Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni mjini Dar es Salaam, mabao ya Samuel Kamuntu dakika ya 51 na Najim Magulu dakika ya 73.
JKT Tanzania iliyorejea msimu huu Ligi Kuu, imenusurika kushuka baada ya kumaliza na pointi 47 katika nafasi ya 10, wakati Stand United imemaliza nafasi ya 18 kwa pointi zake 44, ikiungana na Mwadui kwenda kucheza na timu za Daraja la Kwanza kuwania kubakki Ligi Kuu.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO
Coastal Union 0-0 Singida United.
Mbeya City 0-0 Biashara United.
Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC.
Ruvu Shooting 1-0 Alliance FC (Fully Zullu Maganga 25’ p) . .
JKT Tanzania 2-0 Stand United (Samweli Kamuntu 51’, Najimu Maguli 73’).
Ndanda SC 1-3 Mwadui FC (Kigi Makasi : Ottu Joseph 39’, 41’, Salim Aiyee 61’) .
Yanga SC 0-2 Azam FC (Daniel Amoah 45’+2, Mudathir Yahya 50’).
Mbao FC 1-1 Kagera Sugar (Hebert Lukindo 60’ : Ally Ramadhan 20’).
Tanzania Prisons 3-1 Lipuli FC (Benjamini Asukile 29’, Adam Adam 48’, 85’ : Seif Rashid 46’).
African Lyon 0-2 KMC FC (Cliff Buyoya 21’, 17’)