*********************
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
September 6
MKUU wa Mkoa wa Pwani,alhaj Abubakari Kunenge , ameeleza hatokuwa tayari kumfumbia macho yoyote atakaebainika kuhujumu wananchi kwa kukwamisha utekelezaji wa bajeti na kuacha miradi kuwa viporo hali inayosababisha kurudisha fedha Serikali kutokana na udhaifu huo.
Aidha ,amekemea kujiingiza katika miradi ili kuhakikisha unapata chochote kwani kwa kufanya hivyo ni kuwacheleweshea wananchi maendeleo.
Kunenge alitoa rai hiyo ,katika kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2021/2022,mkataba wa lishe ,;miongozo ya elimu na tathmini ya ukusanyaji wa mapato ,kikao ambacho kimefanyika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa, Kibaha.
Mkuu huyo wa mkoa ambae alikuwa ni Mwenyekiti wa kikao hicho ,alieleza wananchi wanawapima kulingana na kutatua kero zinazowakabili , lazima wajipime ,wajipange kupata matokeo chanya.
“Kama utekelezi bajeti ,utakuwa unakwamisha huduma za maendeleo “;!Rais Samia Suluhu Hassan anatupatia mafungu ya fedha za kutosha, hatuwatendei haki wananchi, Tunaletewa fedha halafu mwisho wa mwaka miradi haitekelezwi na fedha zinabaki” Inapaswa tuwajibishane,Hatuwezi kuwaacha !!alisisitiza Kunenge.
Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu, Mkoani Pwani, Rukia Muwango alieleza, Mwaka wa fedha 2022/2023 mkoa wa Pwani fungu 71 umeidhinishiwa bajeti ya sh.335,110,456,000 kati ya kiasi hicho sh.206,063,824,000 ni ruzuku ya matumizi ya kawaida,sh.80,568,294,000 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na sh.48,478,338,000 za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Hata hivyo alifafanua, bajeti ya mkoa wa Pwani kwa mwaka 2022/2023 imeongezeka kwa sh.36,279,573,000 sawa na asilimia 12.14 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2021/2022.
Rukia alielezea ,Ongezeko hilo limetokana na mishahara kwa asilimia 19.38, matumizi mengineyo (OC) asilimia 21.82 , fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo asilimia 9.44 na mapato ya ndani ya Halmashauri asilimia 23.33.