Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo “ASA” Dkt.Sophia Kashenge akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya Pro Agro Global Ltd ya Jijini Arusha Bryson Maro walipokuwa wanasaini mkataba huo
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo “ASA” Dkt.Sophia Kashenge akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya Pro Agro Global Ltd ya Jijini Arusha Bryson Maro wakibadilishana mikataba ya ujenzi wa miundombinu ya umwangiliaji na aliyesimama katika kati yao ni mwanasheria wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Wakili Valentine Kamugisha
……………………………………
Na Lucas Raphael,Morogoro
Wakala wa Mbegu za kilimo “ASA” umesaini Mkataba wa kufunga miundombinu ya Umwagiliaji katika Hekari 2016 za mashamba yaliyupo katika mikoa ya Tabora ,Arusha na Morogoro
Wakala umeingia mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji na Kampuni ya Pro Agro Global ltd ya Jijini Arusha wenye thamani ya shilingi Billion 18.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika hafla fupi ya kusaini Mkataba huo iliyofanyika makao Makuu ya Wakala, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo “ASA” Dkt.Sophia Kashenge amesema Mkataba huo ni utekelezaji wa maelekezo ya wizara ya kilimo wa kuhakikisha Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo unakuwa wa uhakika usiotegemea mvua.
Amesema mashamba yatakayo pitiwa na Mradi huo ni pamoja na Shamba la Msimba lililopo Kilosa Mkoani Morogoro Hekta 200 sawa na Hekari 500, Shamba la Arusha Ngaramtoni Hekta 200 sawa na Hekari 500 pamoja na Shamba la Kilimi Nzega Hekta 400 sawa na Hekari 1000.
Dkt.Kashenge amesema ufungaji wa miundombinu hiyo utaongeze Uzalishaji wa Mbegu kwa msimu mzima wa mwaka tofauti na Sasa mashamba yote ya Wakala Uzalisha Mbegu ufanyashughuli za kilimo kwa msimu Mmoja.
Aidha Mtendaji huyo Mkuu wa Wakala alisema utekelezaji wa Mradi huo unaanza uwekaji wa miundombinu hiyo muda usiopungua miezi 10 Kama Mkataba unavyosema.
Amesema katika Mkataba huo kuna baadhi ya maeneo ya kuchimba visima na mabwawa ambapo Shamba la Msimba Morogoro ni uchimbaji wa Visima na bwawa,Shamba la Arusha Ngaramtoni uchimbaji wa Visima na bwawa huku Shamba la Kilimi Nzega uwekaji wa miundombinu ya Umwagiliaji Kutokana na uwepo wa bwawa la Kilimi lenye maji ya kutosha.
Dkt.kashenge ameipongeza serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu kwa kuwa na kiu kubwa ya mabadiliko ya kilimo kutoka kilimo Cha kutegemea mvua hadi kilimo Cha umwagiliaji.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya Pro Agro Global Ltd ya Jijini Arusha Bryson Maro ameipongeza serikali kwa kuendelea kuamini makampuni ya wazawa ambapo hawa yalikuwa hayaaminiki.
Amesema kulingana na Mkataba ulivyo kazi hiyo itaanza Mara moja ilikuhakikisha kila kitu kinakwenda Kama kilivyo pangwa ndani ya Mkataba huo.
Amesema Kama vijana wa kitanzania watahakikisha wanafanya kazi vizuri pasipo kwenda nje ya Mkataba ilikuendelea kuaminika kwa serikali.
Kwa upande wake mwanasheria wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Wakili Msomi Valentine Kamugisha amesema Mkataba huo umefuata taratibu zote za kisheria hadi kufikia hatua ya kuweka Saini kwa pande mbili zote.
Kamugisha amesema nimatumaini ya Serikali kuwa pande zote mbili zitafuata taratibu na kanuni zilizowekwa ilikufikia malengo ya Serikali ya kuweka miundombinu kwa mashamba yote ya Uzalishaji wa Mbegu za kilimo.