Makamu Mkuu wa Chuo ,Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Emmanuel Luoga (Kulia) na Mkuu wa kanda ya Afrika ICDL Peter Maina (Kulia) wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Ujuzi wa kidigitali wenye lengo la kuongeza ufanisi katika ufundishaji katika ukumbi wa mkutano wa taasisi hiyo Tengeru Arusha Septemba 2, 2022.
Makamu Mkuu wa Chuo ,Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Emmanuel Luoga (Kulia) na Mkuu wa kanda ya Afrika ICDL Peter Maina (Kulia) wakibadilishana hati ya Mkataba wa Makubaliano ya Ujuzi wa kidigitali mara baada ya kuweka saini katika Ukumbi wa Mkutano wa taasisi hiyo Tengeru Arusha Septemba 2, 2022..
Wajumbe waliohudhuria hafla ya kuweka saini Mkataba wa Makubaliano ya Ujuzi wa kidigitali baina ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Utoaji wa Vyeti vya Kompyuta ( ICDL Afrika) wakifatilia uwasilishajia wa Taarifa kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo ,Profesa. Emmanuel Luoga (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mkutano wa taasisi hiyo Tengeru Arusha Septemba 2, 2022.
Mhadhiri kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Sanket Pandhare (wa pili kulia) akielezea utendaji kazi wa Kompyuta yenye Utendaji wa Juu (HPC) kwa Mkuu wa Kanda ya Afrika ICDL Peter Maina ( wa pili kushoto) na Mratibu wa ICDL Tanzania Edwin Masanta (wa kwanza Kushoto) walipotembelea Maabara ya Kompyuta ya Taasisi hiyo wengine ni Bi. Grace Kija (wa nne kulia),Dkt . Zeeshan Khan (wa tatu kulia) na Dkt. Efraim Kosia ( wa kwanza Kulia) leo Septemba 2,2022.
Makamu Mkuu wa Chuo ,Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Emmanuel Luoga (Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja Mkuu wa kanda ya Africa ICDL Peter Maina (Kushoto) na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Profesa. Kelvin Mtei(kulia) mara baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano ya Ujuzi wa kidigitali na Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Utoaji wa Vyeti vya Kompyuta (ICDL Afrika) katika ukumbi wa Mkutano wa Taasisi hiyo Tengeru Arusha Septemba 2, 2022.
……………………………………
Na Mwandishi Wetu,Arusha
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) imesaini Mkataba wa Makubaliano ya Ujuzi wa kidigitali, na Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Utoaji wa Vyeti vya Kompyuta (ICDL Afrika) kwa lengo la kuongeza ufanisi katika ufundishaji.
Akizungumza katika halfa hiyo, Septemba 2, 2022 jijini Arusha, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa. Emmanuel Luoga amesema Taasisi hiyo imeona umuhimu wa kushirikiana na Taasisi ya ICDL Afrika ili kuleta umahiri na ufanisi wa kazi, na kujenga uwezo wa kidijitali kwenye nyanja mbalimbali za kimaendeleo na kielimu katika kukuza sekta ya mawasiliano nchini .
Profesa Luoga ameeleza kuwa, taasisi hiyo itakuwa na mtandao wa mawasiliano ya teknolojia ikiwemo Kituo cha Umahiri katika kuhakikisha masuala ya mawasiliano yanakwenda kasi kuendana na utandawazi.
“Tunataka chuo chetu kiwe cha kwanza katika umahiri na utoaji ujuzi wa kidijitali katika masuala ya kompyuta” amesema Profesa Luoga.
Naye Mratibu wa ICDL nchini Tanzania, Ndg. Edwin Masanta amesema wameamua kushirikiana na taasisi ya Nelson Mandela katika kuhakikisha wanaongeza utendaji kazi na ufanisi kwa kutoa mafunzo ya elimu ya kidigitali kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu kielimu.
Aidha, amesema kuwa, Tanzania ya viwanda ni lazima iweze kuendana na kasi ya teknolojia ya kompyuta katika kuhakikisha ubora wa maendeleo unaendana na kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kutumia kompyuta.
Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Taasisi ya Nelson Mandela kwa niaba ya Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala Profesa Kelvin Mtei amesema programu hiyo ya kompyuta itaongeza tija ya ufanisi na utendaji kazi katika kukuza uchumi.