Naibu Rasi ,Taaluma,Utafiti na Ushauri elekezi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dkt.Christina Raphael akizungumza katika warsha ya wadau wa mradi wa Utafiti wa ‘Spaces’ ambayo imefanyika leo Septemba 1,2022 katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Jijini Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi idara ya Jografia na Uchumi, Mtaalamu wa Mazingira Dkt.Emiliana Mwita akizungumza katika warsha ya wadau wa mradi wa Utafiti wa ‘Spaces’ ambayo imefanyika leo Septemba 1,2022 katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Jijini Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi idara ya Jografia na Uchumi, Mtaalamu wa Mazingira na Elimu ya Mazingira Dkt.Daniel Sabai akizungumza katika warsha ya wadau wa mradi wa Utafiti wa ‘Spaces’ ambayo imefanyika leo Septemba 1,2022 katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Jijini Dar es Salaam. Afisa Mazingira Mwandamizi -NEMC, Bi.Kulthum Shushu akizungumza katika warsha ya wadau wa mradi wa Utafiti wa ‘Spaces’ ambayo imefanyika leo Septemba 1,2022 katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Jijini Dar es Salaam. Naibu Rasi ,Taaluma,Utafiti na Ushauri elekezi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dkt.Christina Raphael akipata picha ya pamoja na wadau wa mazingira katika warsha ya wadau wa mradi wa Utafiti wa ‘Spaces’ ambayo imefanyika leo Septemba 1,2022 katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Naibu Rasi ,Taaluma,Utafiti na Ushauri elekezi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dkt.Christina Raphael amewataka watafiti katika Chuo hicho kuhakikisha wanatumia utafiti wao kutatua changamoto ambazo zinaikabiri jamii hasa kwenye suala zima la kutupa taka za plastiki kwenye maeneo yasiyo sahihi.
Ametoa wito huo wakati akifungua warsha ya wadau wa mradi wa Utafiti wa ‘Spaces’ ambayo imefanyika leo Septemba 1,2022 katika Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Jijini Dar es Salaam.
Amesema kwa vile vyuo vikuu vya kimataifa vinashiriki katika utekelezaji wa utafiti huo, hakuna shaka kwamba matokeo yanaweza kupitishwa kwa urahisi na nchi mbalimbali duniani kama hatua za kuzuia utupaji wa plastiki usio rafiki.
“Tunaelewa kuwa utafiti utafanyika Mto Msimbazi hapa Dar es Salaam lakini nataka nisikilize matokeo hayo yatoe ufumbuzi wa kudumu kwa maeneo yote ya nchi kwa sababu tatizo la utupaji ovyo wa plastiki linaonekana kila mahali,”. Amesema Dkt.Christina
Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi wa Idara ya Jiografia na Uchumi wa DUCE, Dkt.Emiliana Mwita amesema katika zoezi hilo wamejipanga kuanzisha mambo kadhaa yanayosababisha utupaji ovyo wa taka za plastiki.
“Mradi huu unalenga kuweka njia nzuri za jinsi ya kutupa taka za plastiki bila kuhatarisha maisha ya watu na mazingira kwa ujumla ikizingatiwa kuwa kuna changamoto nyingi zinazojitokeza iwapo taka ngumu hasa plastiki hazitatupwa ipasavyo,” Amesema Dkt.Mwita
Amesema mradi huo utafanyika kwa awamu nne ambapo ya kwanza ikiwa ni kutafuta chanzo cha plastiki hizo, jinsi zinavyoingia nchini, kwa nini watu wanazitumia na hatima yao ya mwisho.
Nae Mhadhiri Mwandamizi idara ya Jografia na Uchumi, Mtaalamu wa Mazingira na Elimu ya Mazingira Dkt.Daniel Sabai amesema takribani taka za plastiki milioni 800 zinatupwa maeneo mbalimbali na zinabeba vimelea kama mbu na vimelea ambavyo vinasababisha homa ya denguna magonjwa ya TB.
Hata hivyo kwa upande wake Afisa Mazingira Mwandamizi -NEMC, Bi.Kulthum Shushu amesema wameendelea kusimamia katazo la mifuko ya plastiki ambayo imekatazwa na walitoa kanuni za usimamizi wa mazingira ambapo wameendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha wanachi wanakuwa na uelewa mkubwa kuhusu athari za matumizi ya mifuko ya plastiki.