Naibu Waziri wa Afya Dr.Godwin Mollel akizungumza na Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano Bohari Kuu ya Dawa MSD Bi. Etty Kusiluka wakati alipotembelea Katika Banda la Bohari hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya Dr.Godwin Mollel akimsikiliza Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano Bohari Kuu ya Dawa MSD Bi. Etty Kusiluka wakati alipotembelea Katika Banda la Bohari hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya Dr.Godwin Mollel akifurahia jambo na Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano Bohari Kuu ya Dawa Bi. Etty Kusiluka pamoja na Wafanyakazi wa Bohari hiyo wakati alipotembelea Katika Banda la Bohari hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
……………………………………
Naibu Waziri wa Afya Dr.Godwin Mollel ameishauri Bohari ya Dawa (MSD) kutengeneza mpango wa muda mrefu wa kuzungumza na wawazalishaji dawa na bidhaa nyingine za afya kutoka nchi zinazozalisha bidhaa hizo kuja kuwekeza nchini Tanzania,hatua ambayo itarahisisha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.
Naibu waziri ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa MSD pia iangalie namna ya kuingia mikataba na nchi zinazozalisha bidhaa za afya kurahisisha kununua moja kwa moja kutoka kwao, ili kupunguza gharama na kuwezesha kupata bidhaa za kutosheleza mahitaji.
Kiongozi huyo pia amewahimiza wazalishaji hao wa nje kuja kuwekeza nchini Tanzania kwa kuingia ubia na serikali.