****************************
Na Lucas Raphael,Tabora.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawalisiano Tanzania (TCRA),Dkt Jabir Bakari amesema kwamba Sensa ya mwaka huu itaonesha shughuli za biashara ambazo awali zilikuwa hazijulikani na Mamlaka ya Mawasiliano,TCRA.
Alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza katika kikao cha wadau wa sekta ya Mawasiliano kutoka mikoa ya Kigoma,Dodoma,Siginda na Tabora kilichofanyika kwenye ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani hapa
Mkurugenzi huyo mkuu wa TCRA,Dk alisema kuwa Sensa ya mwaka huu ina umuhimu zaidi kwa vile itaonesha biashara ambazo huenda hzikuwepo hapo awali .
Alisema kutokana na biashara kufanyika kidigitali ,kunasababisha hata wafanyabiashara nao kubadilika kwani wasipobadilika watakufa kibiashara.
Alisisitiza kwa wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa kuwa wabunifu ili kuendana na wakati na ushindani wa kibiashara ambao ni mkubwa kwa sasa.
Dkt Jabir akiongeza umuhimu wa Sensa baada ya kupatikana takwimu,alisema zitaonesha watoa huduma wingi na mahitaji na huduma na hivyo kulazimika kupeleka huduma sehemu husika.
Aliongeza kuwa kwa sasa wameongeza utaalamu na wanaweza kubaini mambo yanayofanyika katika anga la Tanzania na maeneo mbalimbali hadi wilayani.
Dkt Jabir Alieleza kuwa mkoa wa Tabora wenye eneo kubwa na kuongoza nchini,una idadi kubwa ya watu na matokeo ya Sensa,yataonesha hata mahitaji yake kuongezeka tofauti na kipindi hiki.