***********************
NA MWANDISHI WETU
KAMISHNA Msaidizi Ustawi wa Jamii, Mstaafu Donald Charwe, amewataka wanachama wa kikundi cha WADAU 2017, kuwaheshimu viongozi ili watimize malengo ya kuwa taasisi ya fedha.
Charwe alitoa wito huo, wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho, Pugu, Dar es Salaam, jana, ambapo alisema viongozi na wanachama lazima wazingatie katiba yao pamoja na mambo wanayoazimia katika vikao vyao.
Alisema ili watimize malengo ya kikundi hicho cha kuinuana kiuchumi pamoja raha, lazima waheshimiane na kufuata katiba yao kikamilifu.
“Mimi siwaiti nyinyi ni kikundi, bali mimi nawaita nyinyi ni umoja ambao mna malengo mazuri ya kuinuana kiuchumi pamoja na kupeana furaha, pia baada ya kuwa kikundi mtakuwa taasisi kubwa ya fedha, mtakaoweza kuondoa matatizo ya watu na kuweka furaha”, alisema.
Pia Charwe alisema uwepo wa kikundi hicho kitasaidia kuondoa dhana na uharifu katika maeneo yao, kwani muda mwingi watakuwa wakijadili mambo ya maana pamoja kupeana furaha.
Naye Katibu wa WADAU 2017, Isack Tenga, alisema malengo yao ni kuponya mioyo ya watu pamoja na kuinunuana katika nyanja ya kichumi kwa miongoni mwao na waliokuwa nje ya kikundi hicho.
Alisema malengo yao yatafanikiwa endapo kutakuwa na ushirikiano wa kutosha, ili baadaye wawe taasisi kubwa ya kifedha barani Afrika na kusaidia jamii.
“Mimi ni Katibu wa kikundi hichi cha WADAU 2017 nitayasimamia yote tuliyoazimia katika vikao na kufuata katiba yetu na kutoa ushirikiana ili tufike mbali. Pia kikundi kina malengo mzuri ya kustawiaha maisha kiuchumi kwa wanachama wa kikundi na waliokuwa nje ya kikundi na kuponya mioyo ya watu”, alisema.
Naye Mtunza Fedha msaidizi wa kikundi hicho, Caroline Kisamo, alisema kikundi hicho kina utofauti na vikundi vingine kutokana na malengo yao waliojiwekea ili kuyafikia mafanikio yao.
“Kikundi chetu kinatofauti na vikundi vingine, ambavyo vimejikita katika kusaidiana au kuchangiana wakati wa misiba, ila sisi ni kusaidiana kuinuana kiuchumi pamoja na raha”, alisema.