Mchezaji wa Mapinduzi FC akiwa amebeba kikombe mara baada ya kuibuka washindi wa mashindano ya utalii cup
Wachezaji wa Mapinduzi FC wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa MZFA, FRAKI pamoja na mgeni rasmi ambae ni Afisa mwandamizi wa utalii
Daines Kunzugara Afisa utalii mwandamizi akiwa ameshikilia kikombe kwaajili ya kuwakabidhi Mapinduzi FC
**************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mapinduzi FC waibuka washindi katika mashindano ya utalii cup yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Mmashindano hayo yamemalizika Jana Agositi 27,2022 ambapo mshindi wa kwanza Mapinduzi FC alipata zawadi ya shilingi milioni 5 pamoja na kikombe huku mshindi wa pili Copco Fc alipata milioni 3,mshindi wa tatu milioni moja na nusu na mshindi wa nne alipata milioni 5.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Afisa utalii mwandamizi Daines Kunzugara alisema mashindano hayo yamekuwa chachu katika Mkoa wa Mwanza kwa kuhamasisha vijana kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo kisiwa cha sanane.
Kunzugara ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuwa wazalendo kwa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Mkoani hapa.
Akizungumzia siri ya ushindi wa Mapinduzi FC kocha wa timu hiyo Magogo Mataba,amesema kuwa wachezaji wameonyesha uwezo wao wa kucheza kwa kutulia katika kipindi chote cha mashindano.
“Timu yangu iko kwenye dalaja la chini lakini wachezaji wako dalaja la juu na wanauwezo wa kucheza ligi dalaja la kwanza,la pili pamoja na ligi kuu”,alisema Magogo
Francis Shao, ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Fraki ambao ndio walikuwa wadhamimini wa mashindano hayo kwa kushirikiana na MZFA alisema mashindano hayo waliyaanzisha kwa lengo la kuhamasisha jamii kufanya utalii wa ndani pamoja na kuleta hamasa ya utunzaji wa misitu,uoto wa asili na vyanzo vya maji.
Naye Katibu Mkuu wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) Leonard Malongo,alisema mashindano hayo yamefikia malengo kwa asilimia 90 huku akisema kuwa wanatarajia kufanya vizuri zaidi msimu ujao.