****************
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 15 kwa ajili ya kununua magari yatakayo
pelekwa kwa Makamanda wa Polisi wa mikoa na kwa Ma Ocd pamoja na fedha ya
mafuta itakayokwenda moja kwa moja wilayani ili kurahisisha utendaji kazi za
Polisi.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya Polisi Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amewataka askari wahitimu kuwaheshimu Watanzania
ikiwa pamoja na kutenda haki sambamba na kuyashughulikia matukio ya uhalifu kwa
wakati na kwa haraka.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura amesema kuwa hadi sasa
hali ya nchi ni salama na ina amani na utulivu wa kutosha ikiwa bado Jeshi hilo
linaendelea kudumisha hali hiyo kwa kushirikiana na wananchi, vyombo vingine
vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya utoaji haki.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya
Polisi Tanzania SACP Ramadhani Mungi amesema shule ilipokea zaidi ya wanafunzi
4310 na waliohitimu mafunzo hayo 4122 huku wengine 186 wakiachishwa mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo utovu wa nidhamu.
Aidha, wahitumu hao wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya
nadharia na vitendo.