Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla akizungumza katika kikao kazi na Viongozi wa Masoko, Machinga na Maafisa Masoko wa Jiji la Dar es Salaam,kikao ambacho kimefanyika leo Agosti 24,2022 Mkurugenzi wa NEMC, Dkt.Samwel Gwamaka akizungumza katika kikao kazi na Viongozi wa Masoko, Machinga na Maafisa Masoko wa Jiji la Dar es Salaam,kikao ambacho kimefanyika leo Agosti 24,2022 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Rehema Madenge akizungumza katika kikao kazi na Viongozi wa Masoko, Machinga na Maafisa Masoko wa Jiji la Dar es Salaam,kikao ambacho kimefanyika leo Agosti 24,2022Mkurugenzi anyesimamia Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira-NEMC, Mhandisi Redemka Samweli akizungumza katika kikao kazi na Viongozi wa Masoko, Machinga na Maafisa Masoko wa Jiji la Dar es Salaam,kikao ambacho kimefanyika leo Agosti 24,2022 Baadhi ya Viongozi wa Masoko, Machinga na Maafisa Masoko wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika kikao na Mkuu wa Mkoa pamoja na NEMC kujadili ni namna gani wanaweza kuondokana na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini, kikao hicho kimefanyika leo Agosti 24,2022. Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao kazi na Viongozi wa Masoko, Machinga na Maafisa Masoko wa Jiji la Dar es Salaam,kikao ambacho kimefanyika leo Agosti 24,2022 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akiwa kwenye kikao kazi na Viongozi wa Masoko, Machinga na Maafisa Masoko wa Jiji la Dar es Salaam,kikao ambacho kimefanyika leo Agosti 24,2022
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***********************
– Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango Ameelekeza msako wa mifuko ya Plastiki ufanyike Mikoa yote.
– Awataka Viongozi wa Masoko yote kutoa tangazo la katazo la uuzaji wa Mifuko hiyo.
– Wenyeviti wa Masoko waahidi kushirikiana na Serikali kwenye Operesheni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza operesheni ya kukamata Mifuko ya plastiki iliyokatazwa kuanza rasmi Jumatatu ya August 29 kwenye Masoko yote ya Mkoa huo.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kazi na Viongozi wa Masoko yote ya Mkoa huo, Machinga na Maafisa Masoko ambapo pia ameelekeza msako wa kukamata Viwanda Bubu vinavyozalisha Mifuko hiyo kuanza Mara moja.
Aidha RC Makalla ameelekeza kila Wilaya kupitia Kamati za Ulinzi na usalama kuendesha Operesheni hiyo ambapo pia amewataka Maafisa Masoko kwa kila soko kutoa taarifa ya mwenendo wa zoezi Hilo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika kila siku.
Tayari RC Makalla amepata baraka zote za Operesheni hiyo kutoka kwa Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango ambae ameelekeza kila Mkoa kufanya Operesheni ya kutokomeza na kuzuia uingiaji wa Mifuko hiyo.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Mamlaka za Udhibiti ikiwemo Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC na TBS kutoa tamko la maelekezo ya usimamizi kwa kila Mkoa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Elimu inaendelea kutolewa.
Itakumbukwa kuwa mnamo tar 01/06/ 2019 Serikali ilitangaza marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya plastiki na kufanikiwa lakini hivi karibuni Mifuko hiyo imeanza kurudi kwa Kasi jambo lililopelekea Serikali kutangaza Operesheni ya kutokomeza.
Nae Mkurugenzi wa NEMC, Dkt.Samwel Gwamaka amekiri vifungashio vya plastiki kurudi kwa nguvu pamoja na jitihada kubwa wanazozifanya za kuvidhibiti kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
” Kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki kuna nchi hazijaweka zuio la mifuko ya plastik hivyo inaingia nchini kupitia mipakani. Kwa hiyo tunapata changamoto nyingi Kanda ya Ziwa, mikoa ya Kaskazini, Kusini na Magharibi. Tatizo limezidi kuwa kubwa kwa kuwa vifungashio hivi vinavyoingia sokoni tunapambana na mifuko rahisi kwa Gharama ndogo,” Amesema