*************************
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameeleza ,pamoja na Halmashauri ya Chalinze watahakikisha Mji huo unaendelea kuwa wa kisasa na kuvutia kwa wageni, wawekezaji na wanaopita Mjini hapo kuelekea mikoa ,na nchi jirani.
Akitembelea Mzunguko wa makutano ya Barabara Bwilingu, Chalinze kuona kazi inayoendelea kupendezesha sura ya Halmashauri hiyo yapo waliyoshauriana ili kuifanya kazi iliyokwisha fanywa kuwa Bora zaidi.
Ridhiwani ameeleza, makutano hayo ndio kioo Cha Chalinze,ambapo kitaeleza baadhi ya vitu vinavyopatikana Chalinze ili iwe chachu mwa jicho kwa wanaopita Mjini humo.
Amesema ,kwasasa Chalinze inaendelea kupiga hatua ya kimaendeleo na kiuchumi siku Hadi siku ,hivyo inafaa makutano ya barabara hiyo ambayo magari yanakwenda maeneo mbalimbali ivutie na kuonyesha sura nzuri .