Mkufunzi Ofisa Mpango wa Chanjo Fat-hia Said Bedui akiwasilisha mada ya Elimu ya Chanjo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua Rubel na Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano itakayofanyika Uzinduzi wake tarehe 26 hadi 30/09/2019 Kivunge Mkoa wa Kaskazini A Unguja
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt,Fadhil Mohamed Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua Rubel na Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano itakayofanyika Uzinduzi wake tarehe 26 hadi 30/09/2019 Kivunge Mkoa wa Kaskazini A Unguja.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt,Fadhil Mohamed Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua Rubel na Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano itakayofanyika Uzinduzi wake tarehe 26 hadi 30/09/2019 Kivunge Mkoa wa Kaskazini A Unguja.
*********************************
Na Rahma Khamis Maelezo 19/9/2019
Jamii imetakiwa kuwa tayari kuwapeleka watoto kupatiwa Chanjo ya kitaifa dhidi ya maradhi ya Surua Rubella na Polio ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na maradhi hayo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Fadhil Mohammed Abdalla wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Wizara ya Afya .
Amesema kuwa endapo jamii itajitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo hiyo itawakinga na madhara mbalimbali ikiwemo kupoteza baadhi ya viungo na kupelekea ulemavu .
Aidha amefahamisha kuwa kampeni ya chanjo hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 26 mwezi huu huko Kivunge Mkoa wa Kaskazini A’ na zoezi hilo litaendelea kwa siku tano hadi tarehe 30 ambapo itawalenga zaidi watoto kuanzia umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano ambao ndio waathirika zaidi wa maradhi hayo.
Nae Mkufunzi wa Kampeni ya Chanjo ya maradhi ya Surua Rubella na Polio Fathiya Saidi Bedui amesema lengo la kampeni hiyo ni kuzuwia na kupambana na maradhi yanayozuwilika kwa chanjo .
Amesema maradhi ya Surua na Rubella chanjo yake kuanzia miezi 9 hadi miaka mitano ambapo Polio kuanzia miezi 18 hadi 48 hivyo jamii iwapeleke watoto wao katika chanjo hiyo ingawa wameshawahi kupatiwa chanjo hiyo ili kupata chanjo zaidi.
Akifafanua dalili za maradhi ya Surua na Rubella Mkufunzi Fathiya amesema kuwa mtoto kuwa na homa kali kuchuruzika mafua macho kuwa mekundu na kumwaga machozi hivyo akina mama wanapoona hali hiyo wafike katika Vituo vya Afya kwa uchunguzi zaidi.
Wakijibu maswali Mratibu wa Chanjo za mama na mtoto Yussuf Haji Makame na Afisa Mipango wa Chajo Zanzibar Abdulhamid Amour Saleh wamesema iwapo
itatokea kupooza kiungo kwa ghafla cha mtoto kufikisha Hospitali kwa haraka ili kujulikana tatizo.
Wamesema kuwa ugonjwa wa Surua na Rubella hauna chanjo maalum hukingwa na chanjo ya Surua na Rubella hivyo ikitokea mtoto kupata maradhi hayo anatakiwa kupewa chakula na maji ya kutosha .
Wakizungumzia suala la vifaa vya chanjo hiyo wamesema kuwa tayari vimeshakamilika na kusambazwa sehemu husika hivyo wanajamii waachane na dhana potofu na kuwapeleka watoto wao katika chanjo hiyo.
Kampeni ya Chanjo ya Surua Rubella na Polio itashirikisha Hospitali zote za SerIkali na binafsi na sehemu maalum ambazo zimeteuliwa kwa shughuli hiyo.