************************
OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Waziri Bashungwa ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumza na wananchi wa Makambako mkoani Njombe wakati Rais Samia aliposimama kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
Amesema “Mhe. Rais tumetekeleza maagizo yako ya kutangaza zabuni za ujenzi wa barabara zinazotekelezwa chini ya TARURA mapema ili waweze kuanza kazi hizo kabla ya msimu wa mvua kuanza na tumefanya hivyo kwa mwaka huu na Tarehe 14.08.2022 Wakandarasai walioshinda zabuni hizo watakua wanasaini mikataba yao.
“Tunakushukuru kwa kuridhia kuja kushuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo ya TARURA ambayo utekelezaji wake itakwenda kufungia mawasiliano ya barabara vijijini na mjini kwemye Halmashauri zote nchini,”amesema.
Amebainisha kuwa kwa Halmashauri ya Makambako, bajeti ya TARURA imeongezeka kwa asilimia 250 kutoka Sh.Milioni 800 walizokuwa wanapata hapo awali mpaka Sh.Bilioni 2.8 wanazopata hivi sasa.
“Kutokana na ongezeko hili ndio maana Mhe. Mbunge anashukuru kwa Mabilioni ndio kama haya sasa ya TARURA waliyopata, na kupitia Mradi wa kupendezesha Miji 48 wa TACTIC Mji huu utaweza kujengewa Stendi, Soko la kisasa na maeneo ya kupumzikia ili Mji huu uweze kupendeza kama ili hali ya hewa ya hapa,”amesema.