Mkurugenzi mtendaji mpya wa UTPC Keneth Simbaya akizungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya (CRPC) hawapo pichani alipotembelea Ofisi zao maili moja Kibaha.
********************
Na Victor Masangu,Pwani
Mkurugenzi mtendaji mpya wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya ameahidi kushirikiana bega kwa bega na klabu zote kwa lengo la kuweza kuleta mapinduzi na mabadiliko chanya katika tasnia hiyo ambayo yatasaidia waandishi kuheshimika na sio vinginevyo.
Kauli hiyo ameitoa leo Agosti 10 wakati alipotembelea Ofisi ya klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Pwani(CRPC) na kupata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji kwa lengo la kuweza kubadilishana mawazo kwa lengo la kuboresha zaidi klabu zao.
Simbaya pia ameweza kugagua ofisi hiyo pamoja na kujionea vitendea kazi mbali mbali ambavyo vinatumiwa na waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani katika kuanda habari zao na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuijenga tasnia ya habari hapa nchini.
“Kikubwa mm leo tangu nichaguliwe ndio klabu hii ya waandishi Mkoa wa Pwani ndio nimekuja kuwatembelea ingawa nitafanya ziara yangu rasmi ya kuweza kukutana na viongozi wote pamoja na wanachama kwa hivyo nimefarijika kukutana na waandishi wenzangu ambao tumefanya nao kazi kwa kipindi kirefu tangu nikiwa Rais wa UTPC,”alisema Simbaya.
Pia alisema licha ya kutembelea ofisini pia lengo lake lingine kubwa ni kuhakikisha kwamba anaweka mikakati ya kuleta mabadiliko chanya katika klabu za waandishi wa habari kwa kuwaongezea ujuzi wa kozi mbali mbali ambazo zitawafanya waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Kadhalika aliongeza kuwa kitu kikubwa ni kuwa wavumilivu na kutokukata tamaa katika utekelezaji wa kuhabarisha umma na kwamba inapaswa kujifunza zaidi na kuangalia nini ambacho akistahili kukifanya na nini ambacho kinastahili kuanza nacho ili kutimiza malengo.
Kwa upande wake Katibu wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Pwani Gustaphu Haule pamoja na mratibu Charles Kusaga wamesema lengo lao ni kufika mbali zaidi hivyo wanahitaji sapoti kutoka kwa uongozi wa UTPC ikiwemo kuwapatia mafunzo ya aina tofauti ambayo yataweza kuwa mkombozi katika sekta ya habari.