************************
NA FARIDA SAID, MOROGORO
WAKALA wa huduma za Misitu Tanzania TFS Kanda ya Mashariki imewataka watanzania kuwa na muamko wa kufanya utalii wa Kikolojia kwa kutembelea maeneo yalio hifadhiwa pamoja na maporomoko ya maji yanayohifadhiwa na mamlaka hiyo katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikwemo yale yanayopatikana katika Mkoa wa Morogoro.
Hayo yamebainishwa na kamanda wa TFS kanda ya mashariki,Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Caroline Malundo wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara ya kutembelea maporomoko ya maji Hululu kwenye hifadhi ya mazingira asilia ya Ulugulu iliyochini ya wakala hiyo katika kijiji cha Vinile Wilaya Mvomero Mkoani Morogoro
Alisema katika msitu huo kuna vivutio mbalimbali vya utalii ikwemo ndege kwenye sauti nzuri zenye kuvutia, panzi mwenye rangi nne za bendera ya Taifa, maua ya senti paulia, kima weupe pamoja na vinyonga wenye pembe mbili,moja na pembe tatu ambao wamekuwa kivutio kikubwa katika msitu huo
Pia alisema katika kanda ya mshariki kuna vivutio vingi ukwemo msitu wa utete unaopatikana Rufiji mkoni Pwani,msitu wa mazingira asilia wa Mkingu uliopo Wilayani Mvomero pamoja na msitu wa hifaddhi wa kimboza unapatikana wilaya ya Morogoro na Mkoa wa Morogoro na misitu mingine inayopatika katika Mkoa wa Tanga.
Aidha aliwata watanzania kuunga mkoono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suruhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana na katika hifadhi mbalimbali zikiwemo hifadhi za misitu na maporomoko ya maji yalio chini ya TFS.
“Pamoja na kujionea lakini tunawakalibisha watanzania kuja kupunzika katika hifadhi zetu kwani wanapofanya kazi ngumu kwenye hali ya hewa ambayo sio nzuri kutokana na mwingiliano wa watu na viwanda, basi maeneo yetu ya misitu ya hifadhi ni maeneo ambayo yanaweza yakajenga afya zao, kwa hiyo tunawakaribisha wote waweze kutembelea hifadhi zetu.” Alisema Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Malundo
Aidha alisema TFS Kanda ya Mashariki imefanya uwekezaji mkubwa katika maeneo yote ya utalii yanayopatikana katika kanda hiyo ili kutoa nafasi kwa watanzania na wasio watanzaia kuweza kufanya utalii wa ikolojia katika maeneo hayo.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mazingira asilia ya Ulugulu Benadetha Chile aliesema ziara hiyo ilihusisha watalii wa ndani 34 waliotembelea banda la TFS kanda ya mashariki na kupata ofa ya kutembelea vivutio vilivyopo katika hifadhi ya mazingira asilia ya Ulugulu ambapo walipata fursa ya kujionea maporomoko ya maji ya Hululu pamoja na utalii wa ikolojia.
Alisema pamoja na maporomoko ya maji ya uhululu ambayo yamekuwa kivutiuo kikubwa cha watalii kuweza kutembelea msitu huo pia kuna kivutio cha uwanda wa lukwangule ambacho ni chanzo kikuu cha maji ya Mto ruvu.
Nao watalii waliotembelea hifadhi ya mazingira asilia ya Ulugulu na maporomoko ya maji ya Hululu walisema wamefurahishwa sana na utalii wa ikolojia kwani wameweza kujionea viumbembalimbali, sauti nzuri za ndege zenye kuvutia,vinyonga pamoja na kuvuta hewa safi kwenye msitu huo kabla ya kufika kwenye maporomoko ya maji ya hululu.
Aidha wamwataka watanzania wengine ambao bado hawajafika katika msiti wa hifadhi ya mazingira asilia ya Ulugulu na maporomoko ya maji ya hululu kufika kutembelea ili wajionea uzuri wa asili wa msitu huo.