Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi mbalimbali wakifurahi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA kilichojengwa Wilayani Ikungi mkoani Singida.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa veta, Anthony Kasole (kushoto) akimuelekeza jambo Waziri Mkuu Kassi Majaliwa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Chuo cha VETA.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Iglanson, kilichopo katika Wilaya ya
Ikungu, akiwa kwenye ziara ya siku moja mkoani Singida.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amekagua miradi ya maendeleo na kuweka jiwe
la msingi la ujenzi wa kituo cha afya cha Iglanson, Chuo cha Mafunzo ya Ufundi
Stadi Veta na Hospitali ya Wilaya ya Ikungi vyote vikiwa wilayani humo mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kikazi ya
siku moja.
Akikagua ujenzi wa kituo cha afya Iglanson na kuweka jiwe la msingi la
kituo hicho jana Waziri Mkuu, Kassim
aliuagiza uongozi wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida kuhakikisha ujenzi wa
kituo hicho kilichopo jimbo la Singida
Magharibi unakamilika ifikapo mwishoni mwa Agosti mwaka huu ili kiweze kuanza
kutoa huduma kwa wananchi.
Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wanannchi wa kata ya
Iglansoni katika ziara yake ya kukagua miradi hiyo ya maendeleo inayotekelezwa
wilayani humo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho ambacho
serikali ilishatoa zaidi ya Sh.milioni 500.
“Mhandisi simamia kumalizia jengo ili mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti
huduma zianze kutolewa mara moja ili wananchi waondokane na adha ya kutembea
umbali wa zaidi ya kilometa 100 kufuata huduma za matibabu Singida mjini na
Itigi,” alisema.
Majaliwa alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi, Justice Kijazi,
pamoja na kwamba rais ametoa kibali cha ajira za madaktari watakaoletwa kwa
ajili ya Wilaya ya Ikungi waletwe moja kwa moja katika kituo cha afya
Iglansoni.
“Jengo nimeliona limekamilika kwa asilimia 98 sasa huduma za upasuaji
zitafanyika hapa hapa hakutakuwa na sababu ya kutembea umbali mrefu kwenda
Singida au Itigi kufuata huduma,” alisema.
Waziri Mkuu alisema serikali italeta fedha nyingine Sh.milioni 250 kwa
ajili ya kujenga wodi ya wanaume na wanawake,mochwari na kujenga nyumba za
kuishi madaktari watakaokuwa wakitoa huduma katika kituo hicho cha afya.
Aidha,alisema katika magari ya kubebea wagonjwa (ambulance) ambayo serikali
itahakikisha moja linaletwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambalo
litakuwa linatoa huduma kwenye kituo cha afya Iglansoni kwa wagonjwa wanapewa
rufaa kwenda hospitali ya wilaya Ikungi.
Kuhusu ombi lililotolewa na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu,la
kutaka jimbo hilo lipewe Halmashauri kwa kuwa ni kubwa kwani wananchi wamekuwa
wakitembea urefu za zaidi ya kilometa 200 kufuata huduma katika Halmashauri ya
Wilaya ya Ikungi.
Majaliwa aliwagiza viongozi kufuata taratibu zote zinazotakiwa kwa kuitisha
vikao kuanzia ngazi za chini hadi juu na kupeleka mapendekezo na ikimpendeza
rais ambaye ndiye mwenye mamlaka na hilo atatoa maelekezo ya kuanzishwa
halmashauri mpya katika jimbo la Singida Magharibi.
Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
David Silinde, alisema serikali imeshatoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya
ujenzi wa vituo vya afya 234 nchi nzima.
Alisema katika mkoa wa Singida serikali ilitoa Sh.bilioni 13.3 kwa ajili ya
ujenzi wa madarasa 667 katika shule za sekondari na msingi.Awali Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,Justice Kijazi, alimweleza Waziri Mkuu kuwa
serikali imetoa Sh.milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya
ambacho kitatoa huduma kwa wananchi 13,608 wa vijiji vya Iglansoni na Mnyange.
Alisema changamoto iliyojitokeza katika utekelezaji wa mradi huu ni pamoja
na upatikanaji wa vifaa ambavyo vilikuwa vinapatikana katika umbali wa zaidi ya
kilometa 100 na tatizo la maji smbapo pipa moja lilinunuliwa kwa Sh.500 hali
ambayo imesababisha kuongezeka kwa gharama za ujenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro, alisema serikali imetoa fedha kwa
ajili ya ujenzi wa vituo vinne vya afya pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ambayo imepewa Sh.milioni
800.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa fursa kwa wabunge wa
maeneo ilipo miradi hiyo kuzunngumzia miradi hiyo inayotekelezwa kwa kutolewa
fedha nyingi na Rais Samia Suluhu Hassan.
Wabunge waliopata fursa hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi,
Elibariki Kingu ambako kimejengwa kituo cha Afya cha Iglanson, Mbunge wa Jimbo
la Singida Mashariki Miraji Mtaturu ambako kimejengwa chuo cha Ufundi Stadi cha
Veta na Hospitali ya Wilaya.
Wabunge wngine waliopata fursa hiyo ni pamoja na Mussa Sima Mbunge wa
Singida mjini na Mbunge wa Viti Maaalum Mkoa wa Singida, Martha Gwau na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, JUuma Killimbah..