Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida , Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Ivo Ombella akizungumza wananchi kuhusu moto uliozuka Benki ya NMB mjini hapa leo.
Ulinzi ukihimalishwa.
Mkuu wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) Mkaoa wa Singida, Yowabu Lusatila, akizunguza na wananchi kuhusu moto uliozuka Benki ya NMB mjini hapa leo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida limefanikiwa kuuzima moto uliozuka katika Benki ya NMB mkoani hapa umbao ulitokea kutokana na hitilafu ya umeme.
Akizungumza na wananchi eneo la tukio Mkuu wa Kikosi hicho mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Ivo Ombella alisema katika tukio hilo wamefanikiwa kulidhibiti pamoja na mali zilizokuwemo katika benki hiyo pamoja na fedha.
Alisema majira ya saa nne asubuhi walipigiwa simu kujulishwa kuhusu moto huyo ambapo walifika na kuudhibiti na kuwa watumishi watatu wa benki hiyo walijeruhiwa katika tukio hilo na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kipatiwa matibabu.