Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule,akipokelewa na watumishi wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwasili katika ofisi zake mpya baada ya kuhamishiwa Dodoma na kutoka Mkoa wa Geita leo Agosti 4,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi zake mpya baada ya kuhamishiwa Dodoma akitokea Mkoa wa Geita leo Agosti 4,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule,akiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka wakisaini nyaraka kabla ya kukabidhiana Ofisi leo Agosti 4,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule,akiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka wakikabidhiana nyaraka za Ofisi leo Agosti 4,2022 jijini Dodoma.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka,akizungumza maa baada ya kumkabidhi Ofisi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule makabidhiano hayo yamefanyika leo Agosti 4,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akimpongeza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka ambaye amehamishiwa Mkoa wa Njombe kwa kazi aliyoifanya na kuahidi kuendeleza majukumu hayo mara baada ya kukabidhiwa Ofisi hiyo leo Agosti 4,2022 jijini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga,akizungumza mara baada ya kumpokea Mkuu wa Mkoa Mpya wa Mkoa huo Rosemary Senyamule leo Agosti 4,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Wakuu wa Wilaya pamoja na watumishi wa Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka ambaye amehamishiwa Mkoa wa Njombe leo Agosti 4,2022 jijini Dodoma.
……………………………
Na Eva Godwin-DODOMA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amehaidi kuyaendeleza yale ambayo ameyaacha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka kwa kuzingatia kanuni na sheria za kazi.
Ameyasema hayo Leo Agosti 4,2022 wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma Mh.Anthony Mtaka Jijini Dodoma.
Amesema Atatekeleza na kufanya yale aliyoyafanya mtaka kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote .
“Ntayaendeleza uliyofanya na uliyoyahaidi kwa kuzingati sheria ya kazi na nimeona Mmefanya kazi kubwa na nimethibitisha kwa hizi dokumenti ambazo mmenikabidhi.
“Nimeona kazi mlizofanya chini ya Mwaka Mmoja lakini Mmenikabidhi mpango kazi kuanzia 2021-2022 na 2023-2025 inamaana ndio umeanza utekelezaji hivi karibuni mmenifanya sasa kuwa mwepesi na kujiona sina kazi kubwa ya kutafakari nini cha kufanya kwasababu teyari kilakitu kimeshawekwa kwenye mpango mkakati wa miaka mitano (5) kazi yangu kubwa tu ni kufanya sasa haya yatokee yasibaki kwenye makaratasi”.Amesema Senyamule
Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka afanya amesema Katika Mikoa ambayo amefanya kazi Dodoma ni Mkoa wa Kipekee tangu ameingia katika utendaji wake wa kazi, kutokana na uchapakazi kutoka kwa watendakazi pamoja na ushirikiano uliopo kutoka Mkoani humo.
“Nina marafiki wengi kutoka Serikalini lakini nimefanya kazi na Fatma ni Mtu mzuri na ni raha sana kufanya kazi na mtu mwenye roho nzuri kwasababu anajua wajibu wake bila kupelekeshwa”,amesema Mtaka
“Kwa hiyo Mh. Rosemary unakatibu ambae ni Material kwa kitu chochote ambacho utamuagiza kwasababu ukifanya kazi na Mtu mwenye roho nzuri na ofisi yenu inakuwa yenye maendeleo na ni Mtu ambe ni mshirikishaji sana”.Amesema Mtaka
Ameongezea kwakusema Mkoa wa Dodoma ni Mkoa wenye matamanio sana Na kuna fursa nyingi kwa Wanafunzi wenye degree kufanya kazi kwa kujitolea.
“Vijana ambao Mungu hajawapa hajira wa vyuo vikuu nilijitahidi kuwapa fursa wapate nafasi ya kujitolea kwenye ofisi yetu na wakati mwingine niliona nijambo ambalo linaweza likawakwaza sana lakini walijitahidi
“kwasababu ukiwauliza wanakwambia hawajawai kujitolea sehemu yoyote kwaio nilazima wajitolee ili wajekuingia kwenye mfumo wa kazi na ninajua hili Mh.Rosemary utaliendeleza”.Alisema Mtaka
Naye Katibu Tawala Mkoa Wa Dodoma, Fatma Mganga,amesema kuwa Mkoa wa Dodoma unaumoja kutokana na Mtaka alijitahidi kuweka kila Mdau kwa kila tukio.
“Mh.Rosemary Mkoa wa Dodoma tunaumoja wa hali ya juu na hii inatokana na Mh.Mtaka kuwapa kipaumbele wadau kila kwenye tukio na ndio maana leo umekaribishwa na jopo la Watu wengi hapa Jinini Kwetu”,amesema
“Hii ni Mbegu ambayo ametuachia sisi Wanadodoma na katika kufanya kazi pia tunashirikiana vizuri sana kwaio hili ni jambo tu la kumpongeza Mh.Mtaka”.Amesema Mganga
Amesema Kama kiongozi hujajipanga katika Mkoa huu utakuyumbisha kutokana na Ukubwa wa Mkoa wa Dodoma
“Mkoa wa Dodoma ni Mkubwa sana kwaio kama kiongozi hujajipanga Mkoa unaweza kukuyumbisha na pia tunamshukuru tu Mungu kuna viongozi mahari katika Mkoa wetu kuanzia wakurugenzi,Wakuu wa Wilaya
“Na sisi hatujawai kuwa Namba za Ajabu katika kila endiketa ya Nchi hii na ninavyozungumza hapa Sisi Dodoma ndio tumeongoza katika chanjo ya Uviko 19”.Amesema