Bw. Semu Mwakyanjala-Afisa Mawasiliano Mwandamizi Mkuu kutoka Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, akitoa Elimu na msaada kwa wananchi waliofika katika banda la TCRA kwenye Maonesho ya Kilimo-Nane Nane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoa wa Mbeya.
Kauli mbiu “Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.”
Wananchi kutoka viunga mbalimbali vya jiji la Mbeya wakiwa wamekusanyika mbele ya Banda la Maonesho la TCRA kupata maelezo na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya mawasiliano. TCRA inatumia fursa ya Maonesho ya NaneNane kutoa elimu ya usalama wa mawasiliano na mitandaoWananchi kutoka viunga mbalimbali vya jiji la Mbeya wakiwa wamekusanyika mbele ya Banda la Maonesho la TCRA kupata maelezo na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya mawasiliano. TCRA inatumia fursa ya Maonesho ya NaneNane kutoa elimu ya usalama wa mawasiliano na mitandaoWananchi kutoka viunga mbalimbali vya jiji la Mbeya wakiwa wamekusanyika mbele ya Banda la Maonesho la TCRA kupata maelezo na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya mawasiliano. TCRA inatumia fursa ya Maonesho ya NaneNane kutoa elimu ya usalama wa mawasiliano na mitandao
Mhandisi John Asajile-Meneja wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, akitoa Elimu na msaada kwa wananchi waliofika katika banda la TCRA kwenye Maonesho ya Kilimo-Nane Nane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoa wa Mbeya.
Kauli mbiu “Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.”
**************************
Banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) limekuwa kimbilio la watumiaji wa huduma za Mawasiliano, kwenye Maonesho ya Wakulima Nane Nane, yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
TCRA ni moja ya taasisi zaidi ya 320 zinazoshiriki katika maonesho hayo ya Wakulima ya Nane-Nane ambayo kitaifa yanafanyika Mbeya Mwaka huu. Banda ya TCRA katika maonesho hayo limekuwa kivutio ambapo Ufumbuzi wa changamoto zote za watumiaji wa huduma za mawasiliano hutolewa hapo (One stop Centre).
Watumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu wenye changamoto mbali mbali, wanapata ufumbuzi wa matatizo yao moja kwa moja kwenye banda la TCRA ambapo Kampuni zinazotoa huduma ya simu za mkononi wote wako hapo, zikiwemo Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Airtel, Vodacom, tIGO na Halotel.
Wananchi kutoka sehemu mbali mbali za Nchi wanaomiminika kwenye banda la TCRA, pia wanafaidika na elimu ya matumizi bora na salama ya mitandao, ikiwemo mambo muhimu ya kuzingatia unapotumia huduma za mawasiliano.
Katika kutoa elimu hiyo, Meneja wa TCRA, Kanda ya Nyanja ya Juu Kusini Eng. Asajile John ameshauli wananchi wanapopata ujumbe wa kitapeli, kwa mfano, “Ile pesa tuma kwenye namba hii, Usipige Simu imeharibika spika”. Tuma Namba ya aliyekupigia au kukutumia Ujumbe wa Kitapeli kwenda 15040 BURE.
Wananchi wanatakiwa kuwa makini wanapotumia huduma za mawasiliano ili kuepuka wizi, ulaghai na utapeli. Unatakiwa Kuhakiki Idadi ya Laini za simu zilizo Sajiliwa kwa Kutumia Namba ya Kitambulisho chako cha Taifa Kutoka NIDA, kwa Kubofya, *106#, arafu, utaona namba 1 hadi 5, kwenye Ujumbe wa simu yako. Na. 1. Angalia Usajili 2. Namba zilizosajiliwa na NIDA yako. 3. Namba Zilizosajiliwa Mitandao Yote kwa NIDA yako, 4. Kufuta Usajili, 5. Kuhakiki au Kuongeza Namba.
Meneja wa TCRA, Kanda za Nyanja za Juu Kusini Mhandisi Asajile John pia alielezea wananchi utendaji kazi wa Mtambo wa Utambuzi na Upimaji wa Masafa, (Mobile Frequency Spectrum Monitoring Station), pamoja na Kifaa ha Upimaji wa Mionzi ya Mawasiliano (Electric and Magnetic Field Radiation Metre), ambapo kilionesha mionzi ikiwa chini kabisa ya viwango, kwahiyo salama kwa Wananchi na watumiaji wa huduma.
Zaidi ya laini za simu milioni Hamsini na Nne (54milioni), zinatumika nchini kote, ambapo mawasiliano ya meshawafikia zaidi ya asili mia 90 ya wananchi. Zaidi ya milioni therasini na mbili (32 milioni) wanafaidika na huduma ya kutuma na kupokea pesa, na wengine 32 milioni wapo kwenye huduma za mtandao wa inteneti.
Utafiti uliofanywa na Umoja wa Afrika (African Union) hivi karibuni umebainisha kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wa Kwanza kwa Ubora kwa Nchi ya Afrika Mashariki na Kati nay a Pili kwa Ubora kati ya Nchi 52 Barani Afrika.
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, alizinduwa maonesho hayo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Nane-Nane Kitaifa Mkoani Mbeya, Tarehe 01/08/2022, na kuhimiza Taasisi za Utafiti wa Teknolojia ya Kilimo na Bidhaa zake, kuongeza ubunifu kwa ajili ya tija na ufasini, katika sekta ya Kilimo hapa Nchini.