Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango akipata maelezo juu ya matumizi bora ya mbegu za kisasa kutoka kwa Mtaalamu kutoka kampuni ya Sedco Ltd ,Franko Frederick katika viwanja vya nanenane Njiro.
Mtaalamu kutoka kampuni ya uzalishaji mbegu,utafiti na uuzaji wa mbegu ya Kibo Seeds Ltd,Franko Frederick akizungumza katika maonyesho hayo jijini Arusha.
…………………………………..
Jackline Laizer,Arusha.
Arusha.Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Mhandisi Richard Ruyango ameipongeza kampuni inayohusika na maswala ya uzalishaji ,utafiti na uuzaji wa mbegu ya Kibo Seeds Ltd kwa kutoa elimu kwa wakulima namna ya kilimo bora kinachoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi na hatimaye kuweza kulima kilimo biashara.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati alipotembelea Banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro.
Ruyango amesema kuwa,kitendo cha kampuni hiyo kuendelea kutoa elimu Kwa wakulima juu ya matumizi ya mbegu bora za kilimo kinaleta tija kwao kwani kinaongeza uzalishaji wa mazao na kuweza kulima sehemu ndogo na kupata mazao mengi.
“Nimetembelea Banda hili nimefurahi sana kwa namna ambavyo wakulima wanapata elimu juu ya kilimo bora cha kisasa na matumizi ya mbegu bora ambayo inazalisha zaidi na kuweza kuongeza tija kwa wakulima ambao wamekuwa wakitegemea kilimo katika maswala mbalimbali,hivyo naombeni sana elimu hii iendelee kusambaa zaidi kwa wakulima wengine ambao hawajafikiwa.”amesema.
Mhandisi Ruyango ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha inasambaza elimu hiyo kwa wakulima wengi zaidi ili waweze kunufaika na kuweza kuondokana na kilimo cha mazoea na kuweza kulima kilimo biashara chenye tija ambacho kitawawezesha kuinua kilimo Chao.
Naye Mtaalamu kutoka kampuni hiyo,Franko Frederick amesema kuwa, wataendelea kutoka elimu kwa wakulima wengi zaidi ili waweze kujua mbegu bora za kutumia katika kilimo chao na hatimaye kuweza kupata mazao mengi zaidi na kuondokana na changamoto mbalimbali.
Amesema kuwa,mbegu zao zimekuwa zikienda na wakati kulingana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo wakulima wengi wamekuwa wakinufaika na mbegu hizo ambazo zina uwezo mkubwa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi .
“Mbegu zetu tumekuwa tukizifanyia utafiti kabla ya kupeleka sokoni na zimeleta manufaa makubwa Sana kwani wakulima wameweza kupata mazao mengi katika eneo dogo ,jambo ambalo amewataka wakulima kutumia mbegu za kampuni hiyo ambayo Ina manufaa makubwa kwao.”amesema .
Mmoja wa wakulima ,Asha Musa aliyetembelea Banda hilo na kupata elimu amesema kuwa, ameweza kujifunza namna Bora ya kulima kilimo cha kisasa na katika eneo dogo hali ambayo amesema endapo wakulima watatumia ushauri wa watalaalamu hao wataweza kupata mazao wengi na kulima kilimo cha manufaa.