Naibu Kamishna wa ustawi wa Jamii na huduma za ustawi wa Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi maalumu, Baraka Makona ,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Miaka 25 ya Montessori Community of Tanzania (MCT) likiwa na kauli mbiu isemayo “NISAIDIE NIFANYE MWENYEWE” lililofanyika leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma
Mkuu wa Chuo cha Ualimu PATAJI Montessori Kagera, Kemilembe Ndyamukama ambae pia ni Mwanakamati mtendaji wa Montessori Community of Tanzania,akizungumza kwenye Kongamano la Miaka 25 ya Montessori Community of Tanzania (MCT) likiwa na kauli mbiu isemayo “NISAIDIE NIFANYE MWENYEWE” lililofanyika leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori Community of Tanzania MCT, Sara Kiteleja,akielezea lengo la Kongamano la Miaka 25 ya Montessori Community of Tanzania (MCT) likiwa na kauli mbiu isemayo “NISAIDIE NIFANYE MWENYEWE” lililofanyika leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Kamishna wa ustawi wa Jamii na huduma za ustawi wa Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi maalumu, Baraka Makona (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano la Miaka 25 ya Montessori Community of Tanzania (MCT) likiwa na kauli mbiu isemayo “NISAIDIE NIFANYE MWENYEWE” lililofanyika leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma
Naibu Kamishna wa ustawi wa Jamii na huduma za ustawi wa Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi maalumu, Baraka Makona,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Kongamano la Miaka 25 ya Montessori Community of Tanzania (MCT) likiwa na kauli mbiu isemayo “NISAIDIE NIFANYE MWENYEWE” lililofanyika leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma
…………………………..
Na Eva Godwin-DODOMA
SERIKALI imesema kuwa imesikia Mchango wa Montessori Community of Tanzania na kuutambua kutokana na kazi zake wanazofanya ni jambo kubwa na muhimu kwenye Jamii za Kiafrika
Hayo yamesemwa leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma na Naibu Kamishna wa ustawi wa Jamii na huduma za ustawi wa Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi maalumu, Baraka Makona wakati akifungua Kongamano la Miaka 25 ya Montessori Community of Tanzania (MCT) likiwa na kauli mbiu isemayo “NISAIDIE NIFANYE MWENYEWE”.
Amesema Serikali imesikia Mchango wa Montessori Community of Tanzania na kuutambua kutokana na kazi zake wanazofanya ni jambo kubwa na muhimu kwenye Jamii za Kiafrika
“Hili mnalofanya sio jambo ndogo,nyie mnaweza kuona ni jambo la kawaida lakini kwetu sisi Serikali ni Kitu muhimu na kikubwa kwasababu mnstipikia watoto wakiwa bado wanaumri mdogo mpaka kukua kwa
“Na serikali tunautambua mchango wenu na tunautambua msichukulie hili ni Jambo ndogo, mnavyotumia muda wenu kucheza na watoto mnawaimbia nybo sio jambo la kawaida ni mnatukuzia vyema Taifa letu”.Amesema Makona
Hata hivyo amesema Serikali imeandaa mkakati wa miaka mitano (5) kwaajili ya kuboresha shughuli zote za malezi ya Mtoto na kujumuisha huduma zote za Mtoto kuanzia umri wa mwaka Mmoja (1) hadi nane (8) na makakti huo umeshazinduliwa.
“Na Serikali yetu imeandaa Mkakati wa miaka mitano kwaajili ya kuboresha shughuli zote za malezi ya mtoti na pia tumejumuisha huduma zote za Mtoto kuanzia umri wa mwaka Mmoja hadi miaka 8”,amesema
“Na mkakati huo umeshazinduliwa baadhi ya mikoa hapa Nchini ikiwemo Dodoma na Arusha na pia tunaendelea kuizindua na Mikoa mingine na katika mkakati huo kuna huduma za chanjo, masuala ya lishe kwa mtoto, Tiba na mambo mengine mengi ambayo ni muhimu kwa Mtoto”.Amesema Makona
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori Community of Tanzania MCT, Sara Kiteleja, anasema mbinu ya ufundishaji wa kimontessori ikitumika vizuri, inaweza kumjenga mtoto katika maadili mema ili baadaye aweze kuwa raia mwema wa taifa hili.
“Montessori tunambinu nyingi sana za kumfanya mtoto ajengeke kuanzia kiakili, Kimwili na Kiroho kwaio tukitumia hizi mbinu zetu Watoto wetu watakuwa vizuri na kuwa raia wema katika Taifa letu
“Na Mmeona Serikali yetu imetuamini na inaendelea kutuamini katika utendaji kazi wetu, na bodi hii mpya natumaini tutafanya kazi vizuri kwa uadilifu Kama Serikali yetu inavyosema Kazi iendelee”.Amesema Kiteleja
Naye Mkuu wa Chuo cha Ualimu PATAJI Montessori Kagera, Kemilembe Ndyamukama ambae pia ni Mwanakamati mtendaji wa Montessori Community of Tanzania amemshukuru Naibu Kamishna wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi maalumu kwa kuandaa mikakati ambayo moja kwa moja zinagusa huduma ya Mtoto na Malezi bora.
“Serikali imetambua mchango wetu kwenye jamii na inaendelea kutambua mchango wetu ndio maana pia tumeona mkakati wa miaka mitano (5) kwaajili ya kuboresha shughuli za mtoto ambapo ndani ya hiyo mikakati kuna huduma muhimu za Mtoto”, amesema
“Na pia Mchango wa Serikali ndio umetufanya tufikishe hii miaka (25) pamoja pia na wakongwe wa bodi hii ya Montessori na tusisite kutoa ushirikiano hata kwa mawazo na bodi yetu hii mpya ambayo inaenda kufanya kazi”.Amesema Ndyamukama
Ameongezea kwa kusema Bodi hii ya sasa inatarajia kufanya makubwa hasa kufuata mkakati ulitengenezwa na Serikali kwa kufuata sheria na kanuni zilizopangwa na Montessori.