Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani Ocean road,Dk Julius Mwaisilage akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo kwa niaba ya Waziri wa Afya ,Ummy Mwalimu jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika kongamano hilo jijini Arusha
……………………………….
Julieth Laizer, Arusha
Arusha.Chama cha madaktari bingwa wa maradhi ya Saratani(TOS) kimetakiwa kuhamasisha madaktari waliomaliza masomo na wanaofanya kazi kujiunga katika kusomea programu ya Saratani(oncology) ili kuweza kuondokana upungufu wa madaktari bingwa wa Saratani ambao mpaka sasa wapo 38 nchi nzima.
Hayo yamesemwa Leo jijini Arusha na Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani Ocean road Dkt Julius Mwaisilage wakati akisoma hotuba ya waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika ufunguzi kongamano la kwanza la kimataifa la Saratani lilijumisha wataalamu na wadau ambapo alisema kuwa kutokana na upungufu mkubwa wa madaktari bingwa wa Saratani daktari mmoja kwa mwaka anahudumia wagonjwa 1200.
Dkt Mwaisilage amesema kama chama wana malengo yao lakini kikubwa wahamasishe wataalamu waweze kusomea kwani serikali inatoa ufadhili kila mwaka kwa kupeleka fedha chuo kikuu cha Afya na sayansi shirikishi Muhimbili(MUHAS) hivyo wawahamasishe ili kupunguza upungufu huo.
Aidha amesema kuwa kulingana na takwimu wanazoziona katika hosipitali kwa mwaka wanawaona wagonjwa 14600 sawa na asilimia 33 ambapo idadi hiyo ni ndogo kwani Tanzania ina zaidi ya wagonjwa elfu 42 wa Saratani.
“Mpango wetu ni kuwafikia watumishi wa afya nchi nzima walioko katika ngazi ya mkoa na wilaya katika kuwawezesha wataalamu kugundua ugonjwa huo mapema ili wagonjwa waweze kutibiwa,”amesema Dk.Ndumbaro.
Pia amesema kupitia chama hicho wanampango mkakati wa kufanya huduma za upimaji na ugunduzi wa mapema wa saratani katika jamii ambapo watapita kila mkoa kuhakikisha huduma hiyo inawafikiwa wananchi wa ngazi zote.