Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhi boti sita za uvuvina vifaa vyake kwa kikundi cha wavuvi katika katika Shehia ya Jongoe Kisiwa cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar leo Julai 20, 2022 kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Chilo akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya boti sita za uvuvi na vifaa vyake iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Shehia ya Jongoe Kisiwa cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar leo Julai 20, 2022.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Chilo akishiriki matukio mbalimbali wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye alikabidhi boti sita za uvuvi kwa vikundi vya vya Shehia ya Jongoe Kisiwa cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar leo Julai 20, 2022 kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Chilo akiwa katika boti kutokea Bandari ya Mkokotoni kuelekea Kisiwa cha Tumbatu kushiriki hafla ya makabidhiano ya boti sita za uvuvi kwa kikundi cha Shehia ya Jongoe leo Julai 20 kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
*******************************
Na Robert Hokororo, Zanzibar
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Chilo ametoa rai kwa wanufaika wa mradi wa boti za uvuvi zilizotolewa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) kutofanya shughuli za kibinadamu zinazochangia uharibifu wa mazingira.
Ametoa rai hiyo leo Julai 20, 2022 wakati wa hafla ya makabidhiano ya boti sita za uvuvi zilizokabidhiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Shehia ya Jongoe Kisiwa cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.
Mhe. Chilo alisema boti hizo zitumike kuleta katika tija katika mapambano ya athari za mabadiliko ya tabianchi zinazoikabili nchi yetu na duniani kwa ujumla,hivyo ni wajibu wa wanufaika wa mradi huo kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji, kufanya kilimo endelevu.
Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaendeleza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na ndiyo maana inatekeleza miradi hii.
”Leo zinakabidhiwa boti hizi kwa vikundi vya wavuvi ambao ndio wanufaika wakuu kwa hiyo nitoe rai kwenu mtunze vyanzo vya maji ili viumbe vilivyomo navyo viweze kuishi kutunzwa na mazingira ndio kila kitu kwa vizazi vya sasa na vijavyo,” alisema Chilo.
Aidha, Mradi wa EBARR ni wa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 na unatekelezwa katika Wilaya za Mvomero (Morogoro), Simanjiro (Manyara), Kishapu (Shinyanga), Mpwapwa (Dodoma) Tanzania Bara na Kaskazini A – Unguja, upande wa Zanzibar.
Maeneo ya Mradi yalichaguliwa kwa kuzingatia maeneo yenye ukame yenye jamii za wakulima, wafugaji, na wavuvi kwa lengo la kuongeza uwezo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika jamii za vijijini kwa kuimarisha mifumo ikolojia na shughuli mbadala za kujiongezea kipato.