********************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,alhaj Abubakari Kunenge amewaasa Wafugaji kuachana na ufugaji wa kizamani na kufuga kisasa kwa kufuata utaalamu ili kujiongezea kipato.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Washiriki wa Maonesho na Mnada wa Mifugo yaliyofanyika katika Shamba la Highland Estate lililopo Ubena zomozi Halmashauri ya Chalinze na kuandaliwa na Chama cha Wafugaji Kibiashara (Tanzania Cattle Commercial Society) yaliyoanza kuanzia Tarehe 15 Julai na kuhitimishwa 17 Julai 2022.
Ameeleza, katika Sekta ya Ufugaji ili kupata Tija nzuri lazima kuzingatia mnyororo mzima wa thamani,hivyo Wafugaji wanapaswa kujua malengo yao katika Ufugaji, Aina ya Mifugo wanaotaka kufuga na madawa wanayotumia.
”Kitu chochote bila utaalamu huwezi Kufanya na Kupata Tija hapa kwenye Maonesho haya mtapata taarifa na maarifa zitakazo wasaidia wale waliopo kwenye ufugaji na kwa wale wanaotaka kuingia kwenye ufugaji”
Ameongeza kuwa Matumizi ya Ardhi yameongezeka kwa ajili ya shughuli za kilimo Viwanda madini Makazi, “Binadamu tunaogezeka Mifugo inaongezeka Ardhi bado ni ndogo hivyo lazima tuangalie maeneo tuliyonayo kabla ya kuanza kufuga” Ameeleza Kunenge.
Kunenge amesisitiza , suluhisho la Mgogoro ya Matumizi ya Ardhi ni Ufugaji wenye Tija kutumia eneo dogo, mbegu nzuri zitakazo kupa nyama na maziwa, kufuga mifugo inayohimili maradhi, na kivuna mifugo kwa wakati.
Ametoa Wito kwa watendaj wa Serikali wote kuanzia ngazi ya mtaa kusaidia kuhamasisha Wafugaji kuja kujifunza na kufuga kwa Tija. Amezitaka Taasisi za kibenki zinazoshiriki kusaidia Wafanyabiashara wanapotaka kuwekeza kwenye sekta ya Mifugo.
‘Ni imani yangu tukiboresha sekta ya Mifugo ikawa ni ya uhakika ni rahisi kupewa Bima na kupata Bima ndiyo kupata tija hivyo tutaboresha maisha yetu Tufike mahala mifugo watunufaishe Mifugo watutumikie na siyo sisi kuitumikia mifugo” Ameeleza Kunenge.