Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwasilisha makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dastan
Kitandula akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo leo Bungeni mara bada ya kuwasilisha
makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mbunge wa Muleba Kusini Mhe. Charles Mwijage akichangia hotuba ya makadirio
ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020 leo
Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua akisisitiza jambo kwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Amos Maganga nje ya viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakuu wa Taasisi, Wenyeviti wa Bodi , Watendaji na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo wakifuatilia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara
hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akisisitiza jambo kwa baadhi ya wageni
waliofika Bungeni kwa lengo la kujifunza shughuli za Bunge mapema leo.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akisistiza kuhusu hatua
zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na
huduma ya umeme .
**************************************
Wizara ya Nishati yaomba Kuidhinishiwa Shilingi Trilioni 2.142 ikilinganishwa na shilingi Trilioni 1.692 iliyotengwa kwa mwaka 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 26.6 kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya kuzalisha umeme.
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Waziri wa Wizara hiyo Dkt. M,edard Kalemani amesema kuwa ongezeko hilo linatokana na kuanza kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa Rufiji utakaozalisha megawati 2,115 utakapokamilika.
“ Fedha nyingi za ndani za miardi ya maendeleo zilizotengwa kwa mwaka 2019/2020 zimeelekezwa katika miradi mitatu ya kimkakati ambazo ni shilingi trilioni 1.86 sawa na asilimia95.1 ya bajeti yote ya ndani” Alisisitiza Dkt. Kalemani.
Akifafanua Dkt. Kalemani amesema kuwa miradi hiyo ni; Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Mto Rufiji MW 2,115 uliotengewa shilingi Trilioni 1.44, Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Shilingi Bilioni 363.11 na Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Kinyerezi 1 Extension MW 185 shilingI Bilioni 60.
Aliongeza kuwa Bajeti ya mwaka 2019/2020 inalenga kutekeleza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha kuwa inazalisha umeme wa kutosha, wa uhakikka, unaotabirika na wenye gharama nafuu.
Vilevile, Bajeti hiyo imelenga kuimarisha shughuli za utafutaji na biashara ya mafuta na gesi asilia pamoja na kuwezesha wananchi kunufaika na rasilimali hizo .
Lengo jingine ni kuwezesha ujenzi wa uchumi wa Viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hali itakayosaidia kujenga uchumi jumuishi na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wote hasa wale wanaoishi vijijini.
Akizungumzia upatikanaji wa mafuta hapa nchini Dkt. Kalemani amesema kuwa imeendelea kuimarika kupitia utaratibu wa Serikali kuagiza mafuta kwa pamoja kupitia Wakala wa uagizaji Mafuta kwa pamoja.
“Kati ya mwezi Januari hadi Desemba, 2018 jumla ya lita Bilioni 5.70 za mafuta zilizgizwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara sawa na ongezeko la asilimia 6.3 ikilinganishwa na lita Bilioni 5.36 zilizoagizwa mwaka 2017” Alisisitiza Dkt. Kalemani.
Kwa upande wa usambazaji wa gesi asilia Dkt. Kalemani amesema kuwa wateja 500 wameunganishiwa huduma hiyo katika Jiji la Dar es Salaam hali itakayosaidia kupunguza gharama za maisha kwa wananchi wote watakaoungnishiwa huduma hiyo.
Akizungumzia hatua iliyofikiwa katika kuunganisha viwanda na huduma ya gesi asilia amesema kuwa zoezi hilo linaendelea na viwanda kadhaa vimeshaunganishiwa.