Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akifurahia jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndugu Godwin Mkanwa (kulia) mara baada ya kumaliza hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo kwa Viongozi wa matawi na mashina waliochaguliwa 2022 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jakaya Kikwete Convention.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme akiteta jambo na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Viongozi wa matawi na mashina waliochaguliwa 2022 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jakaya Kikwete Convention.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Viongozi wa matawi na mashina waliochaguliwa 2022 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jakaya Kikwete Convention.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Viongozi wa matawi na mashina waliochaguliwa 2022 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jakaya Kikwete Convention.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndugu Godwin Mkanwa, Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme wakikagua mradi wa vyumba 172 vya maduka vya Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma .
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiweka jiwe la msingi ufunguzi wa mradi wa ujenzi wa vyumba 172 vya maduka katika viwanja vya Barafu Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Picha na Adam H. Mzee/ CCM Makao Makuu)
……………………………
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya wanachama kuanza kujipitisha katika majimbo kutafuta wapambe ili wawasaidia kwenye malengo yao ya Ubunge na udiwani kwa mwaka 2025.
Chongolo ametoa maagizo hayo Julai 13,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Mafunzo ya Uongozi na Itikadi kwa viongozi wa Chama hicho katika Mkoa wa Dodoma, sambamba na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kitega uchumi cha CCM Mkoa wa Dodoma kilichoghalimu zaidi ya shilingi milioni 900 ambapo amesema licha ya kutoa miongozo mbalimbali lakini bado kuna baadhi wanakiuka kwa makusudi.
Chongolo ameonya vitendo vya ukiukwaji wa maadali kwa wagombea mbalimbali wa nafasi za uongozi ndani ya chama hicho huku akiwagiza wasimamizi wa chaguzi hizo kutopitisha majina ya wagombea wote watakaokiuka na kwenda kinyume na miongozo ya chama katika uchaguzi unaoendelea.
”Chama hakitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa taratibu, kanuni na katiba ya CCM ili kuwadhibiti watu hao, kwani muda wa uchaguzi bado na sasa kila jimbo lina mbunge na kila kata kuna diwani hivyo ni vema kwa kila mwanachama kusubiri muda ufike na sio kuanza sasa wakati viongozi waliochaguliwa wanafanya kazi ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.;”amesema Chongolo
Awali Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma bi. Pilly Mmbaga amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo na kuwapa uelewa mbalimbali kwa viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa huku akielezea mwenendo wa uchaguzi ndani ya chama hicho.