Mkurugenzi Mkuu Mpya wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA. Habibu Saidi Suluo ( Upande wa Kulia) akipokea nyaraka za Mamlaka hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Barabara Johansen Kahatano ( kushoto) wakati wa makabidhiano ofisi ya Mamlaka hiyo Jiji Dar es Salaam.
Mkurugenzi mpya wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini(LATRA) CPA. Habibu Saidi Suluo Akiongea na wakuu wa idara na Vitengo (hawapo pichani) wakati makabidhiano ya Ofisi, Suluo aliteuliwa na Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani tarehe 9 Julai ,2022 kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo.
………………………………………..
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migire amemtaka Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA. Habibu Saidi Suluo kuhakikisha wanahamia Dodoma.
Migire ameyasema hayo akiongea wakati wa makabidhiano ya Ofisi katika ya Uongozi uliomaliza muda na uongozi mpya jijini Dar es Salaam na kusema kuwa kuhamia kwao Dodoma kutarahisiha utedaji kwa sasa wanapotakiwa Dodoma hulazimika kusafiri hali inayoongeza gharama za uendeshaji.
“Nikupongeze Mkurugenzi kwa kuaminiwa na kupewa nafasi ya kuongoza Mamlaka hii, nikuagize sasa uharakishe taratibu za kuhamia Dodoma sababu Serikali kuu iko Dodoma na unatambua kuwa maelekezo ya Serikali ni taasisizote makao Makuu yanapaswa kuwa Dodoma’ amesema Katibu Mkuu Migire.
Katibu Mkuu Migire ametumia nafasi hiyo kumtaka Mkurugenzi huyo kuhakikisha anashirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani kudhibiti ajali ambazo zimekuwa zikiongezeka kwenye mabasi na treni.
Aidha, Katibu Mkuu Migire amewataka LATRA kuongeza jitihada katika utoaji wa elimu wananchi na wadau ili waweze kutumia mfumo wa Tiketi Mtandao kwa Urahisi kwani Mfumo huo unasidia kuboresha huduma kwa wanchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA. Habibu Suluo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kumteua kwa nafasi hiyo na kumuhakikishia Katibu Mkuu Migire kuwa atazintaia taratibu, kanuni na miongoz katika uendeshaji wa Mamlak hiyo. ameomba ushirikiano kwa watumishi wa LATRA kwa kufanya kazi kwa Pamoja ili kufikia matarajio ya wananchi.
Mkurugenzi Mkuu CPA Suluo amechukua fursa hiyo kuomba ushirikiano kwa menejimenti na watumishi ili kuwezesha Mamlaka hiyo kufanya vizuri kiutendaji.
Mkurugenzi Mkuu CPA Habibu Suluo amechukua nafasi ya Gilliard Ngewe ambaye amemaliza muda wake.