Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga
Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wa tatu kutoka kushoto na Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Kasim
Kaonekana wa tatu kutoka kushoto wakiwa jezi za traki suti vyenye
thamani ya milioni 2 kwa kwa ajili ya michezo ya Umitashumta iliyoanza leo kwenye shule ya
Sekondari Tanga School
Na Oscar Assenga,TANGA.
MAMLAKA
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa)
imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Milioni 2 kwa ajili ya
michezo ya Umitashumta kwa wanafunzi wa Jiji la Tanga inayoanza leo
kwenye shule ya
Sekondari Tanga School ili kuhakikisha michezo hiyo inafanyika kwa tija
kubwa.
Halfa ya makabidhiano ya vifaa hivyo ilifanyika leo kwenye ofisi za
Mamlaka hiyo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
alimkabidhi Afisa Elimu Msingi wa Jiji hilo Kasimu Kaoneka kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa Tanga
Uwasa Mhandisi Hilly alisema wameamua kutoa msaada huo wa vifaa vya michezo ili
kuweza kuunga mkono mashindano hayo.
Alisema wao Tanga Uwasa kama wadau wa elimu wanatambua umuhimu wa michezo
katika elimu kwa ajili ya wanafunzi ili waweze kupata afya nzuri na kuweze
kusoma vizuri kwa hiyo wamechangia
katika kuhakikisha michezo hiyo inafanikiwa na wanafunzi wanafurahi.
Alisema wanatambua kuwa mazingira bora yanasaidia kuwa na elimu bora
licha ya kuchangia michezo lakini wanachangia ujenzi wa madarasa na viti
vingine ili kutenegenza mazingira mazuri ya elimu.
Awali akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo Afisa Elimu Msingi wa
Jiji la Tanga Kasimu Kaoneka ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Tanga
Spora Liana alisema kwamba michezo ni kitu muhimu kwa wanafunzi kwani wanaenda
shuleni kupata taaluma lakini sio taalima tu ni pamoja na michezo ambacho ni kivutio
kimojawapo kina mfanya mwanafunzi aweze kwenda shuleni.
Alisema na hivyo kupitia
michezo atapata na taaluma yake na hivyo anasisimua ubongo wake hatua
inayopelekea kitu anachofundishwa anakipata
kwa sababu mwili unakuwa upo imara na timamu kiakili.
“Tunawashukuru Tanga Uwasa kwa kutupatia vifaa hivi vya michezo na tunahaidia
kwamba tutahakikisha tunaleta vikombe vingi na tutawakaribisha wakati wa
kukabidhiwa”Alisema
Hata hivyo alisema michezo hiyo ngazi ya Kanda inaanza leo ambapo
itahusisha wilaya za Mkinga,Pangani,Muheza na Tanga na yanafanyika kwenye viwanja
vya shule ya Sekondari Tanga School
Naye kwa upande wake Kasimu Issa anayesoma Darasa la saba shule ya Msingi
majani mapana alisema wanashukuru kwa msaada huo wa vifaa hivyo kuhakidi kwenda
kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.