Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akiongea na wananchi kuhusu umuhimu wa SENSA ya watu na makazi kwa wananchi wa Tarafa ya Pawaga
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kucheza mchezo wa bao mbele ya mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga juu ya umuhimu wa SENSA ya watu na makazi
Baadhi ya wananchi waliojitkeza kumsikiliza mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga juu ya umuhimu wa SENSA ya watu na makazi
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
WANANCHI
wa wilaya ya Iringa wametakiwa kujitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA ili
kutengeneza taswira halisi ya serikali kujua idadi ya wananchi kwa lengo la
kutafuta namna bora ya kuwapelekea maendeleo wananchi kulingana na idadi
iliyopo kila eneo.
Akizungumza
wakati wa sikuku za sabasaba mkuu wa wilaya ya Kahama,Festo Kiswaga alisema
kuwa wananchi watakiwa kujitokeza siku SENSA ili waweze kuhesabiwa kwa ajili ya
maendeleo yao.
Kiswaga
aliwata viongozi mbalimbali kutumia fursa ya uwepo wa michezo kwenye
vijiji,mitaa,kata na tarafa kuhamasisha wananchi wajitokeze kuhesabiwa.
Alisema
kuwa kwenye kila mchezo kunakuwa nakundi kubwa la wananchi hivyo ni rahisi sana
kufikisha ujumbe wa SENSA na ujumbe ukapokelewa vizuri.
Kiswaga
alisema kuwa mchezo wa Bao la solo limekuwa kiunganishi kikubwa kwa wananchi na
serikali kama ambavyo hayati mwalimu Nyerere alitumia mchezo huo katika
harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika na kufaulu kuupata uhuru huo.
Hivyo
michezo yote inatakiwa kupewa kipaumbele sawa ili kuiweka jamii ya wanamichezo
pamoja na kutumia fursa za michezo kwa maendeleo ya taifa.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa umoja wa vijana wilaya ya Iringa vijijini,Makala Mapesa
alisema kuwa mchezo wa bao la solo ni mchezo ambao unachezwa na watu wa lika
zote kwa ajili ya fursa na kutengeneza fursa za kimaendeleo wakiwa wanacheza
mchezo huo.
Mapessa
alisema kuwa mchezo wa bao la solo umekuwa moja ya michezo ambayo unatakiwa
kutumia akiri nyingi na maarifa kuliko kutumia nguvu hivyo ukicheza mara kwa
mara mchezo huo akili yako itachangamka kwenye kufikiri.
Aliowamba
vijana kuucheza na kuenzi mchezo huo wa kitamaduni kwa kuondoa dhana ya kuwa
mchezo huo ni wawazee tu na sio mchezo wa vijana.