***********************
NA EMMANUEL MBATILO
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imewataka Wananchi,Asasi za kiraia na wadau mbalimbali kuendeleza mapambano ya Rushwa katika nafasi walizo nazo kuhakikisha nchi inakuwa na uchumi imara usiohusisha vitendo vya Rushwa.
Akizungumza katika semina ya uhamasishaji na wadau mbalimbali pamoja na Bodi ya ushauri ya maswala ya rushwa katika umoja wa Afrika(AUABC) Kaimu mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo amesema kuwa asasi za kiraia na waandishi wa habari wanamchango mkubwa katika mapambo dhidi ya rushwa na endapo watatumika vyema, rushwa inaweza kutokemzwa na juhudi zinazowekwa katika mapambano zikaamishiwa katika udhibiti pekee.
Aidha, Jenerali Mbungo amesema kuwa TAKUKURU imekuwa mwenyeji wa wajumbe watano wa bodi ya Umoja wa afrika ya ushauri wa maswala ya rushwa ambao wamefika nchini kwaajili ya kufanya tahimini juu ya utekelezaji wa mikataba ya umoja wa Afria katika kupamabana na kuzuia rushwa ambapo ripoti ya awali waliyotoa inaonyesha kuwa Tanzania inamifumo bora ya udhibiti na upamabanaji na rushwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya umoja wa Afrika ya ushauri wa maswala ya Rushwa Bw.BEGOTO MIAROM amesema kuwa Tathimini zinazofanyika katika Nchi wanachama zinapitia katika hatua mbalimbali ikiwa ninpamoja na kuzungumza na wadau mbalimbali juu ya mwenendi wa Udhibitirushwa unavyofanyika na kwa mwenendo wa Tanzania katika uwekaji sheria inaweza kuwa na mifumo itakayotumiwa na nchi nyingine wanachama.
Akitoa taarifa ya bodi ya umoja wa afrika ya ushauri qa maswala ya rushwa kuzuia rushwa Agnes kayobo amesema kuwa mpaka sasa nchi 49 kati ya nchi 55 zimekubali kujiunga na kusaini mkataba huo wa kudhibiti rushwa katika nchi zao huku nchi 14 zikisita kusaini mkata huo hivyi bodi hiyo inaendela na mchakato wa kuzishawishi na kujiunga na kuweza kuwa na malengo ya pamoja katika ncho za afrika ya kutokomeza Rushwa.