Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP Lberatus Sabas amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu mbalimba ikiwemo, elimu ya namna ya kufuga mbwa wa ulinzi, kujua utaratibu wa kumiliki silaha, kufahamu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kupata elimu ya utambuzi wa mabomu. Kamishna Sabas amesema hayo Julai 8, mwaka huu wakati alipotembele Banda la Polisi katika Maonesho ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam.