*************
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,John Mongella amewataka madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Monduli kutokubali miradi inayopelekwa katika kata zao kuchezewa na wakuu wa vitengo kwa lengo la kusababisha wananchi kukosa maendeleo
Aidha ameagiza halmashauri hiyo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato na kuondoa hoja 29 kati ya 55 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Rc Mongella alitoa maagizo hayo jana baada ya kubaini kunabaadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo walibaki na fedha za makusanyo ya ushuru wa minada,na fedha nyingi mkononi bila kuzipeleka benki na wengine kuzipeleka kiasi huku fedha nyingine wakizila
Alisema katika hoja za CAG pia alibaini halmashauri hiyo kushindwa kukusanya mapato hata katika nyumba za wageni ikiwemo fedha za idara ya elimu msingi na sekondari kutopelekwa mashuleni kwaajili ya kupanga shughuli za maendeleo.
Pia aliwaasa madiwani kutokubali miradi inayopelekwa katika kata zao kuchezewa kwani miradi ya maendeleo ikichezewa mwisho wa siku madiwani watapata tabu kuomba kura nyakati za uchaguzi
“Kusanyeni mapato acheni mambo ya ajabu hapa mnawataalam lakini ukimuuliza mtaalam kwanini kunahoja za CAG unaambiwa mfumo umefanya hivi mara vile sasa hizo hela zilizopo kwa watumishi zipo wapi,Mkurugenzi Raphael Siumbu simamia halmashauri hii vizuri napokea vimeseji vingi kuwa upo upo tu huna meno usipoangalia hawa watumishi watakuangusha”
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Isack Joseph alisema halmashauri imepokea maagizo ya Rc Mongella na watahakikisha hoja zenye kasoro zinarekebishwa ikiwemo kuweka timu ya ukusanyaji wa madeni ili kuwezesha utoaji wa mikopo ya asilimia 10kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Huku Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Arusha,Honest Muya aliipongeza Halmashauri hiyo kwakupata hati safi mfululizo kwa muda wa miaka Tisa ingawa bado kunahoja 55 za miaka iliyopita na za mwaka 2020/21 huku hoja 26 zikiwa bado hazijajibiwa,hoja 29 zikijibiwa .
Alitoa rai kwa halmashauri hiyo kuzichambua hoja hizo na kuzirekebisha ili kuhakikisha halmashauri hiyo iweze kujiendesha ikiwemo kungeza kasi ya ukusanyaji wa mapato.