Maafisa Viwango na Wataalamu mbalimbali kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakitoa huduma kwa wananchi ambao wametembelea banda lao katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi wakitembelea banda la Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Julai 03,2022 katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.Maafisa Viwango na Wataalamu mbalimbali kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakiwa tayari kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewakaribisha wafanyabiashara, wenye viwanda pamoja na wananchi kwa ujumla kutembelea banda lao katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 03,2022 katika Maonesho hayo Afisa Uhusiano TBS, Bi.Neema Mtemvu amesema Maonesho hayo yamewawezesha kuwakutanisha na wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kupata huduma mbalimbali kwenye banda lao na kuweza kutatua changamoto ambazo wanakutana nazo wafanyabiashara.
“Kuna wale ambao wanahitaji kufahamu masuala ya Viwango, wanafika hapa tunamuelezea ni namna gani ambavyo ana umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa kuandaa viwango na vilevile kama anataka kiwango ni namna gani anakipata na hapahapa tunaweza kumuwezesha pia akipate”. Amesema
Amesema huduma zote ambazo zimekuwa zikitolewa makao makuu ya TBS au katika ofisi zao za Kanda unaweza ukizipata ukitembelea banda lao katika maonesho hayo ambayo yanayoendelea kwenye viwanja hivyo.