*******************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba imeshindwa kufurukuta mbele ya Tanzania Prisons mara baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Sokoine mkoani Mbeya.
Simba Sc imecheza mchezo huo bila staa wao Sakho ambaye amefanya vizuri kwenye mechi za hivi karibuni kutokana na kupata majeruhi ya bega hivi karibuni na kufanya kukosa mchezo huo ambao haukuwa na faida kwao.
Tanzania Prisons imeshinda mchezo huu na kujiweka eneo zuri kuepuka kushuka daraja hivyo kusubiri mchezo wake unaofuata wa mwisho ambayo itaamua kama wataendela kusali kwenye ligi ama kushuka daraja.
Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na nahodha wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile dakika ya 54 ya mchezo ambaye aliingia kipindi cha pili .