NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe ,akizngumza wakati wa kikao cha wadau wa mapitio ya rasimu ya mwongozo wa kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu hapa nchini kilichofanyika leo Juni 21,2022 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akisisitiza jambo wakati wa kikao cha wadau wa mapitio ya rasimu ya mwongozo wa kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu hapa nchini kilichofanyika leo Juni 21,2022 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Wizara hiyo, Prof. Maulilio Kipanyula, wakati wa kikao cha wadau wa mapitio ya rasimu ya mwongozo wa kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu hapa nchini kilichofanyika leo Juni 21,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi msaidizi Sayansi na Teknolojia Dkt. Alexander Mtawa,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa mapitio ya rasimu ya mwongozo wa kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu hapa nchini kilichofanyika leo Juni 21,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya wadau wakisikiliza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe (hayupo pichani),wakati wa kikao cha wadau wa mapitio ya rasimu ya mwongozo wa kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu hapa nchini kilichofanyika leo Juni 21,2022 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akiwa katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kufungua kikao cha wadau wa mapitio ya rasimu ya mwongozo wa kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu hapa nchini kilichofanyika leo Juni 21,2022 jijini Dodoma.
………………………………………..
Na Alex Sonna – Dodoma.
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia inafanya mapitio ya rasimu ya mwongozo wa kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu hapa nchini huku ikibainisha kuwa hadi sasa wabunifu 2,647 wameibuliwa na kutambiliwa kupitia mashindano ya kitaifa ya Sayansi na Teknolojia na ubunifu (MAKISATU).
Hayo yamebainishwa leo Juni 21,2022 Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe wakati wa kikao cha wadau wa mapitio ya rasimu ya mwongozo huo.
Amesema Mwongozo wa kutambua na kuendeleza ubunifu na maarifa asilia wa Mwaka 2018 umefanikisha
wabunifu 2,647 kuibuliwa ndani ya miaka minne na kwamba mapitio ya rasimu hiyo yanalenga kushiriki wadau na kuibua wabunifu wengi zaidi.
“Tangu uwepo mwongozo huu tumeibua wabunifu wengi tumewatambua wapo 2,647 hawa tumewaibua kupitia mashindano maarufu ya MAKISATU, hawa tumewatambua kupitia mashindano ndani ya miaka minne naamini wapo wengi zaidi ya hao ambao tayari wametambuliwa,” amesema Prof. Mdoe.
Aidha Prof. Mdoe ameeleza kuwa kati ya wabunifu wengi wanaoibuliwa kupitia MAKISATU, pia wabunifu 283 wameendelezwa na wapo kwenye hatua mbalimbali huku zaidi ya 26 bunifu zao zikifikia hatua ya kubiasharishwa.
Akizungumzia wathibiti, Prof.Mdoe amesema shughuli za uthibiti ubora wa bunifu sheria zilizounda mamlaka husika za masuala hayo sio rafiki sana katika kuhamasisha ubunifu.
“Mtu akija na kitu chake cha ubunifu kitu cha kwanza una leseni, umelipia huyu ndo kwanza ameanza kubuni hakijaanza kufanya kazi, atakijaribu vipi wewe unataka alipie ndo ajaribu, lazima tuwe wawezeshaji kuhamasisha ubunifu sio kudhibiti badala ya kuthibiti,”alisema.
Awali Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara hiyo, Prof. Maulilio Kipanyula, amebainisha kuwa lengo la kuboresha mwongozo huo ni kuongeza hamasa, kuibua, kutambua na kuendeleza ubunifu hasa kwa ngazi za chini.
Amesema rasimu ya mapendekezo ya mwongozo huo itajadiliwa na kikosi kazi na kutoa maoni ili kukamilisha mapitio ya mwongozo huo.
Prof.Kipanyula amesema dhamira ya Wizara ni kuhakikisha mwongozo unaboreshwa ili kukidhi mahitaji ya sasa kutokana na mwongozo wa awali ulikuwa na mapungufu ikiwamo kutoonesha majukumu ya wadau katika kuibua, kutambua na kuendeleza wabunifu.