*************************
Na. A/INSP FRANK LUKWARO
Kutokana na kuongezeka kwa matukio na vitendo vya Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji dhidi ya Watoto, Jeshi la Polisi nchini lipo katika hatua za mwisho kulifanya somo la Ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto kuwa somo linalojitegemea katika vyuo vyake ili kukabiliana na vitendo hivyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto, Naibu Kamishna wa Polisi Maria Nzuki wakati wa ufunguzi wa kikao cha kuhuisha mitaala ya Jeshi la Polisi kinachofanyika Shule ya Polisi Tanzania Zamani CCP na kuwashirikisha Wakuu wote wa Vyuo vya Polisi na Kamisheni zote za Polisi.
Kwa upande wao Baadhi ya Wakuu wa Vyuo vya Polisi Wamesema kwa sasa masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji yanafundishwa kwa kiwango kidogo hivyo itakapokuwa somo linalijitegemea itaongeza weledi Zaidi kwa Askari katika kukabiliana na vitendo hivyo.
Kwa Upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la UNICEF Bw. Joseph Matimbwi akitoa mada katika kikao hicho amesema suala la Ukatili ni mtambuka hivyo jamii inapaswa kuungana hususani katika ukatili unaosababishwa na mitandao.