****************************
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alhaj Abubakar Kunenge ,amekagua Maendeleo ya Mradi Sukari (Kilimo cha Muwa na Kiwanda cha Sukari CAKaha Lake Agro Investment Ltd) kilichopo Utete Wilayani Rufiji ,unaotarajia kuzalisha Tani100,000 za sukari kuondoa Nakisi ya sukari kwa nchi na nyingine kuuza nje ya Nchi.
Akizungumza akiwa Eneo la Mradi Kunenge ameeleza wawekezaji hao wapo kwenye matayarisho ya Uwekezaji na kuwa Eneo hilo lina ukubwa wa Hekta 15 ambalo lote litakuwa kwa ajili ya Kilimo cha miwa .
Amesema wawekezaji hao tayari wamejenga njia ya umeme iliyogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 100 na Barabara inajengwa, Matarajio ya Mkoa na Serikali kwa Mradi huo ni kupata Kodi,Ajira ya kutosha zaidi ya watu 18,000 ,Wananchi watapata utaalamu kwa sababu wawekezaji hawa watatumia teknolojia ya kisasa ambayo vijana wetu watajifunza na Mchango wa wawekezaji hao kwa Jamii (CSR).
” Tumekubaliana kwa sababu mradi huu ni Mkubwa paanze kupimwa na kupangwa tupate mji unaojitegemea,tupate Maduka sehemu za huduma za Jamii Masoko na makazi “
“kutakuwa na wakulima wengine wa nje Outgrowers ambapo mwekezaji yupo tayari kuwapa msaada wa kitaalamu ili wachangie kuuza miwa kiwandani”Kunenge alisema.
Naye Mwakilishi wa Kampuni ya Lake Agro Investment Abubakar Nassor amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa Mazingira mazuri ya Uwekezaji na Ushirikiano wanaoupata kutoka Uongozi wa Mkoa.
Ametoa Wito kwa Wananchi kuchangamkia Fursa hiyo kwa Kushiriki kwenye uchumi huu kwa kulima Miwa kwa wale wakulima wa Nje (Out growers) Wafanyabiashara kuleta huduma na kujipatia kipato.