Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akipokea Nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Japan nchini Mhe. Misawa Yasushi leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi Mteule wa Japan nchini Mhe. Misawa Yasushi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Yusuph Mdolwa (katikati), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caesar Waitara pamoja Mkurugenzi wa Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga wakifuatilia uwasilishaji wa nakala za hati za utambulisho za Balozi mteule wa Japan nchini Mhe. Misawa Yasushi
Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Japan nchini wakifuatilia uwasilishaji wa nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Japan nchini Mhe. Misawa Yasushi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wa China anayeshughulikia masuala ya Afrika, Bw. Wu Peng katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wa China anayeshughulikia masuala ya Afrika, Bw. Wu Peng akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (hayupo pichani) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja
………………………………………
Na Mwandishi wetu, Dar
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Japan nchini, Mhe. Misawa Yasushi leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Akipokea nakala ya hati hizo, Balozi Mulamula amemhakikishia Balozi huyo mteule ushirikiano wakati wote katika utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini.
“Nakuhakikishia ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote, naamini tutaendelea kushirikiana katika kukuza na kuendeleza ushirikiano baina yetu kwa masahi ya pande zote mbili kwani uhusiano wa Tanzania na Japan ni wa muda mrefu na umekuwa imara katika kipindi chote,” amesema Balozi Mulamula
Naye Balozi Mteule wa Japan nchini Mhe. Misawa Yasushi amesema atahakikisha uhusiano kati ya Tanzania na Japan unaimarika zaidi na kukua kwa ushirikiano baina ya nchi hizi kupitia nyanja za biashara na uwekezaji na hivyo kunufaisha pande zote mbili.
“Tanzania na Japan zitaendelea kushirikiana kufanya biashara na uwekezaji kwa maslahi ya nchi zote mbili,” amesema Balozi Yasushi.
Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wa China anayeshughulikia masuala ya Afrika, Bw. Wu Peng katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Pamoja na mambo mengine, Waziri Mulamula na mgeni wake, walijadili namna ya kuendelea kuimarisha maeneo ya ushirikiano katika sekta za afya, elimu, bishara na uwekezaji, nishati, miundombinu na usafirishaji.
Bw. Peng ameahidi kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania na kuhakikisha inafanikisha mipango yake ya maendeleo.