Wadau mbalimbali
wa elimu nchini wamebainisha kwamba ili Tanzania iweze kuwa na mfumo wa elimu
jumuishi uliobora kunahitajika ufafanuzi wa kina wa kisera na hapo juu walikuwa kwenye mkutano wa kujadiliana hilo
Wadau mbalimbali
wa elimu nchini wamebainisha kwamba ili Tanzania iweze kuwa na mfumo wa elimu
jumuishi uliobora kunahitajika ufafanuzi wa kina wa kisera
Normal
0
false
false
false
EN-US
X-NONE
X-NONE
MicrosoftInternetExplorer4
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
WADAU mbalimbali wa elimu nchini wamebainisha
kwamba ili Tanzania iweze kuwa na mfumo wa elimu jumuishi uliobora kunahitajika
ufafanuzi wa kina wa kisera pamoja na uwepo wa mikakati madhubuti
itakayotekelezwa kwa vitendo kwenye aina hiyo ya elimu inayolenga kuwaweka
pamoja watoto wenye mahitaji maalumu, kama walemavu, na wale wenye uwezo wa juu
kiakili katika ufundishaji na ujifunzaji.
Kwa mujibu wa internews
Tanzania Mfumo wa ufundishaji unaolenga kuwasaidia na kuwahudumia wanafunzi
wenye mahitaji maalum darasani na utekelezaji kwa vitendo wa utoaji elimu
unaowafanya wanafunzi wote kuwa na thamani katika jamii huo ndio Elimu Jumuishi.
Internews inataja msingi Mkuu wa elimu hiyo jumuishi kuwa ni utu, ubinadamu wa
kuishi pamoja na kushirikiana.
Aidha internews inataja msaada
unaohitajika katika elimu jumuishi kuwa ni pamoja na waalimu wenye uelewa mpana
dhidi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum, utoaji wa msaada kwa wanafunzi wenye
uhitaji maalum, kuwaandaa wanafunzi wasio na uhitaji maalum kuwasaidia na
kushirikiana na wanafunzi wenye uhitaji maalumu.
katika kutambua umuhimu wa
vyombo vya habari Iringa Development of youth disabled and children care(IDYDC) shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa
Inclusive Media Project unaofadhiliwa na
internew Tanzania katika mkoa wa Iringa
kupitia Mratibu wa mradi Reuben Magayane
wanapendekeza jamii ihamasishwe kuhusu umuhimu wa kusomesha watoto wenye ulemavu,mahitaji
maalumu na kuacha tamaduni na imani kuwa watoto wenye ulemavu hawana uwezo na
hawastahili kusoma au kujumuika kwenye jamii.
Magayane alisema kuwa sekta ya
umma na sekta binafsi washirikiane kuhimiza elimu jumishi pamoja na Serikali na wadau wajikite kuondoa vikwazo
vilivyopo, serikali iandae mwongozo kwa lugha nyepesi kwa ajili ya wadau wote,
wakiwemo walimu wa shule/madarasa .
Alisema kuwa serikali
iwekeze katika kuzalisha na kuajiri walimu waliopitia mafunzo ya elimu maalum.”
Pamoja na kupitia upya mitaala ya elimu.Pia kupitia
Taasisi ya Elimu Tanzania serikali ina wajibu wa kufanya maboresho ya vitabu vya elimu pamoja na
kurekebisha na kujenga miundombinu rafiki ili kukidhi mahitaji ya watu wenye
ulemavu na mahitaji maalumu kiujumla
Magayane alesema kuwa kuelekea
sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika kitaifa tarehe 23 agosti 2022
shirika la IDYDC chini ya mradi wa inclusive media project linatoa rai kwa Serikali kuboresha mfumo wa ukusanyaji
takwimu zinazohusu watu wenye ulemavu kwa kuzingatia umri, aina ya ulemavu na
jinsi.Lakini pia IDYDC inapenda kuiasa jamii kushiriki kikamilifu kwa
kuhakikisha watu wote wenye mahitaji maalumu na ulemavu hawaachwi nyuma kwa
kuhakikisha wanashiriki kikamilifu
kwenye zoezi zima la sensa ya watu na makazi kama mwanzo wa kupata
mwarobaini wa changamoto zinazowasibu watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu